Naibu Gavana wa Kilifi Gideon Saburi aachiliwa huru

Mahakama moja mjini Mombasa imetupilia mbali kesi ya kusambaza kimakusudi ugonjwa wa COVID-19 uiliyokuwa imemkabili Naibu Gavana wa Kaunti ya Kilifi Gideon Saburi.

Akitoa uamuzi huo,Hakimu Mkuu, Edna Nyaloti, alihoji kwamba Naibu Gavana huyo hakutangamana kimakusudi na wananchi akiwa na lengo la kuwaambukiza.

Also Read
Raila hategemei kuidhinishwa na Uhuru ili kugombea urais, wasema baadhi ya viongozi wa ODM

Pia alisema wakati wa kushtakiwa kwa Saburi mwaka uliopita, ugonjwa wa COVID-19 haukuwa umetangazwa kuwa hatari wa kuambukiza humu nchini.

Also Read
Kenya yanakili visa 144 vya maambukizi ya korona kutokana na sampuli 2,917

Saburi alikuwa ameshtakiwa kwa kutekeleza uovu huo kati ya tarehe 6 na 22 mwezi Machi mwaka 2020, baada ya kurejea humu nchini kutoka Ujerumani, mojawapo ya nchi zilizokuwa zimeathiriwa na ugonjwa wa COVID-19.

Also Read
Mgombea wa ODM Pavel Oimeke ashinda uchaguzi mdogo wa Bonchari

Alilazimishwa kukamilisha muda wa kuwekwa karantini katika Hospitali Kuu ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani kabla kutiwa nguvuni na maafisa wa usalama na kufunguliwa mashtaka.

  

Latest posts

Serikali yatoa chakula cha msaada kwa wanaokabiliwa na njaa nchini

Tom Mathinji

Daktari aliyewaua wanawe wawili kaunti ya Nakuru amefariki

Tom Mathinji

Shule 43,000 kote nchini kuunganishiwa mtandao wa internet

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi