Naibu Rais William Ruto Kutangaza Mgombea Mweza

Wakati wowote kutoka sasa, Naibu Rais William Ruto ambaye anawania Urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti atatangaza mgeombea mwenza wake. Washirika wa mheshimiwa Ruto walidhibisha kwamba walikuwa wamepokea mwaliko wa kikao cha kutangaza mgombea mwenza kwenye muungano wa Kenya Kwanza hii leo Jumamosi kuanzia saa nne asubuhi katika makazi ya naibu rais huko Karen. Wanahabari walifika huko saa nne asubuhi ambapo wamekita kambi na kufikia wakati wa kuchapisha taarifa hii, hakuna tangazo lilikuwa limetolewa. Waliarifia kwamba kuna mkutano unaendelea kabla ya kikao nao.

Also Read
Washukiwa wawili wanaswa wakisafirisha Misandali ya thamani ya shilingi milioni 12

Tangazo la mgombea mwenza wa muungano wa Kenya Kwanza lilitarajiwa jana lakini likaahirishwa hadi leo. Gavana wa Tharaka Nithi Muthomi Njuki, mbunge wa Chuka/Igambang’ombe Patrick Munene, Didmus Baraza mbunge wa Kimilili na Nelson Koech wa Belgut walithibitisha kupokea mwaliko wa shughuli ya leo.

Also Read
Chama cha DP Chazuiwa kwa Muda

Makataa ya wanaowania Urais kutaja majina ya wagombea wenza na kuyawasilisha kwa tume ya uchaguzi nchini IEBC ni Jumatatu tarehe 16 mwezi Mei mwaka 2022.

Huku haya yakijiri, mgombea Urais wa chama cha muungano wa Azimio la Umoja-One Kenya Raila Odinga naye anatarajiwa kutangaza mgombea mwenza baada ya kamati maalum kutekeleza usaili wa waliokuwa wakimezea mate wadhifa huo kuwasilisha majina ya watu watatu kwake. Huenda akatoa tangazo hilo kesho kwenye mkutano wa kisiasa katika uwanja wa Kamukunji au hata Jumatatu.

Also Read
Philip Subira Anyolo asimikwa kuwa Askofu Mkuu wa jimbo la Nairobi la Kanisa Katoliki

Wanaosemekana kuwa kwenye orodha fupi iliyowasilishwa kwa Raila Odinga ni kiongozi wa chama cha Narc Kenya Martha Karua, Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka na Peter Kenneth mbunge wa zamani wa eneo la Gatanga.

  

Latest posts

Ajali ya kwanza yatokea katika barabara ya Expressway

Tom Mathinji

Rais Kenyatta akamilisha kongamano la Jumuiya ya Madola Rwanda

Tom Mathinji

Waziri Matiang’i: Tutakabiliana vilivyo na makundi ya Majambazi

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi