Naibu wa Rais William Ruto ameahirisha mikutano yake ya umma kudhibiti Covid-19

Saa chache tu baada ya waziri wa Afya Mutahi Kagwe kupiga marufuku mikusanyiko yote, Naibu wa Rais Dkt. William Ruto ameahirisha mikutano yake yote ya umma ilivyokuwa imepangwa hadi itakapotangazwa tena.

Kupitia kitandazi chake cha Twitter siku ya Ijumaa, naibu wa Rais  alisema hatua hiyo  inaambatana na masharti ya kudhibiti msambao wa Covid 19 yaliyotangazwa na serikali, kupiga marufuku mikutano yote ya umma ambayo imelaumiwa kwa kuongeza Idadi ya maambukizi ya Covid-19 hapa nchini.

Also Read
Afrika Kusini yatangaza kanuni mpya za kukabiliana na COVID-19
Also Read
Idadi ya maambukizi ya Covid-19 hapa nchini yashuka

“Tunapaswa kujukumika kibinafsi na kuzingatia masharti yaliyowekwa ili kudhibiti janga hili,” alisema naibu rais.

Waziri wa afya siku ya Ijumaa alipiga marufuku mikutano yote ya umma, ikiwemo mikutano ya afisini akidokeza kuwa serikali imeahirisha mikutano yake ili kudhibiti msambao wa Covid 19.

Also Read
Ongezeko la visa vya Covid-19 nchini,lahujumu ufunguzi wa shule kikamilifu

Waziri huyo wa afya alisema kumekuwa na ongezeko la maambukizi ya Covid-19 katika Kaunti za Kiambu, Kajiado, Lamu, Makueni, Muranga, Taita Taveta na kwa mara ya kwanza katika kaunti ya Tana River.

  

Latest posts

Idadi ndogo ya wakazi wa Nairobi wajitokeza kuchanjwa dhidi ya COVID-19

Tom Mathinji

Watumishi wa Umma wahimizwa kushirikisha taasisi mbali mbali kufanikisha majukumu yao

Tom Mathinji

Kenya yapokea dozi 200,000 za Sinopharm kutoka China

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi