Nandy Aanzisha Kampeni Kwa Jina Funguka

Msanii wa muziki nchini Tanzania Faustina Charles Mfinanga, maarufu kama Nandy ameanzisha kampeni iitwayo “Funguka” ambayo inatokana na wimbo wake wa hivi karibuni kabisa unaofahamika kama “Siwezi”. Anashirikiana na mtangazaji wa kipindi cha XXL cha kituo cha redio cha Clouds Fm aitwaye Mkuwe Issale maarufu kama Mamy Baby ambaye huendesha mpango kwa jina Dada Hood ambao husaidia wasichana na wanawake.

Also Read
Mwili wa Maunda Zorro Kuzikwa Leo

Akizungumza kwenye uzinduzi wa mpango huo Jumatatu tarehe 4 mwezi Aprili mwaka 2022 katika hoteli ya Regency Park, Nandy alisema kwamba yeye kama msanii wa kike ana jukumu la kusaidia vijana wa kike na hata wa kiume katika jamii ili waweze kufunguka na kusema kuhusu changamoto wanazokumbana nazo maishani. Alisema kampeni hiyo itakuwa na mengi ya kufaidi vijana na la kwanza ni seminaa ambayo ilifanyika siku hiyo ya Jumatatu.

Also Read
Ben Pol azungumzia talaka kwa mara ya kwanza

Mamy Baby kwa upande wake alisema aliridhika na wazo alilokuja nalo Nandy ikitizamiwa wimbo wake wa “Siwezi” ambao unaangazia changamoto za kimawazo zinazopata watu wengi kwa sababu ya mapenzi. Alisema lengo lao ni kuhakikisha kizazi ambacho hakina msongo wa mawazo.

Also Read
Mbunge wa Tanzania Zitto Kabwe apata nafuu baada ya ajali

Waliohudhuria kikao cha Jumatatu ni pamoja na mtangazaji wa Clouds Fm Burton Mwemba maarufu kama Mwijaku ambaye aliongoza kikao, Chevawe Kasure mwanzilishi wa wakfu wa Cheliva ambaye anaishi na ulemavu wa ngozi, Nandy na Mamy Baby.

  

Latest posts

Gravity Awataka Bebe Cool na Jose Chameleone Wastaafu

Marion Bosire

Kibao kipya cha Nonini kuzinduliwa siku ya kuzaliwa kwake

Tom Mathinji

Brenda Jons atangaza kuwa sasa ameokoka

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi