Nandy azindua Nandy Festival

Faustina Charles Mfinaga maarufu kama Nandy mwanamuziki wa Bongo ametangaza mwendelezo au ukipenda awamu ya pili ya tamasha lake la mzunguko almaarufu Nandy Festival mwaka 2021. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “watakaa tu” ambayo anasema ina maana kwamba mashabiki wao watakubali kazi ambayo wamewaandalia.

Awamu ya kwanza iliandaliwa mnamo mwaka 2019 ambapo Nandy na wanamuziki kadhaa walizunguka na kupeleka burudani katika mikoa mbali mbali ya Tanzania.

Akizungumza katika mkahawa wa Hyatt Regency jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi hiyo jana, Nandy alielezea kwamba tamasha litaanza tarehe 5 mwezi Juni mwaka huu wa 2021 katika mkoa wa Kigoma.

Also Read
Filamu Ya Mission To Rescue Kuwakilisha Kenya Kwenye Oscars

Alipoulizwa ni kwa nini wamechagua kuanzia huko, Nandy alielezea kwamba eneo hilo limesahaulika kwa muda na wenyeji wana kiu ya tamasha kama hilo.

Msanii huyo alisema kwamba katika mojawapo ya mikoa, wataandaa tamasha la wanawake pekee ambapo kila mmoja atakayehudhuria, atakayetoa huduma au kutumbuiza atakuwa mwanamke kama alivyofanya mwaka 2019.

Nandy Festival mwaka huu, itaandaliwa katika mikoa saba ya Tanzania na katika maeneo mawili ya Kenya hususan Mombasa na Nairobi lakini tarehe sahihi hazikutangazwa.

Also Read
Wasanii wapata Fursa kwenye maonyesho ya SabaSaba

Kuhusu Bilnass ambaye ni mpenzi wake, Nandy alisema ni msanii muhimu sana kwa Nandy Festival kwa hivyo atakuwepo na kwamba hawajawahi kutangaza rasmi kwamba wameachana.

Kwenye bango la uzinduzi wa Nandy Festival kulikuwa na picha ya taulo za usafi kwa kina dada kwa jina “Flowless” bidhaa ambayo Nandy anawakilisha kama balozi.

Mwanamuziki huyo anayefahamika kama “The African Princess” alisema kwamba atahusisha wasanii mbali mbali bila kuangalia kampuni ambazo zinawasimamia kwani wote ni wasanii wa Tanzania.

Also Read
Nandy akana kusajiliwa na Empawa Africa

Aliongeza kwamba hakutakuwa na msanii kutoka nje ya Tanzania kwani ni jukwaa ambalo anaandaa kwa ajili ya wasanii wa Tanzania ambao alisema wanatosha.

Aliulizwa na mwanahabari mmoja kuhusu kiingilio ambapo alisema lazima watatoza ada ya kiingilio kwani kuna vitu vingi vitahitaji hela kama vile kulipia maeneo ya kuandaa tamasha na mambo mengine.

Hakumsahau marehemu John Pombe Joseph Magufuli ambaye alikuwa rais wa Tanzania ambaye alisema alienzi sana wanamuziki huku akipongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa mwanamke wa kwanza kuongoza taifa hilo kama Rais.

  

Latest posts

Arrow Bwoy Amefiwa

Marion Bosire

Shona Ferguson Ashinda Tuzo Hata Baada Ya Kifo

Marion Bosire

Snoop Dogg Atangaza Kifo Cha Mamake

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi