Naseeb Junior Katimiza mwaka tangu kuzaliwa!

Naseeb Junior ni mtoto wa Tanasha Donna mwanamuziki na mtangazaji nchini Kenya na Diamond Platinumz mwanamuziki nchini Tanzania.

Naseeb Junior alizaliwa tarehe mbili mwezi Oktoba mwaka 2019 na siku chache baadaye wazazi wake wakakata uhusiano wa kimapenzi.

Jina lake ni sawa na la babake ambaye anaitwa “Naseeb Abdul”.

Tanasha aliamka mapema,( au tuseme hakulala?) kumtakia mwanawe mema kwenye siku hii yake ya kuzaliwa. Post yenyewe ni kama iliandikwa saa saba usiku.

Tanasha na Naseeb Junior

Bi. Donna amepachika picha akiwa amembeba mwanawe na kuongeza maneno, “Siku kama ya leo, Oktoba 2 mwaka 2019, Allah alinibariki na zawadi nzuri zaidi ya vile ningeomba. Baada ya kuumwa kwa saa 20 hivi, karibu miezi 11 baadaye ulikuwa starehe tumboni mwangu hukutaka kutoka, lakini ghafla ukatubariki na ujio wako ulipoingia ulimwenguni.

Also Read
Agnes amkana Uchebe!

Maneno hayawezi kuelezea jinsi ninajivunia kuwa mama yako, vile ninafurahia kukulea na ninatumai utafurahia sherehe ya kuzaliwa kwako hii leo tunapojumuika kumshkuru Allah kwamba umefikisha mwaka mmoja tangu kuzaliwa.

Wewe ni mwerevu, mkarimu na mwenye utu, unatabasamu kila wakati na mwenye furaha, ulinifunza mapenzi ni nini, ulinifunza kusamehe, ulinifunza kutokuwa na kinyongo, ulinifunza kuwa mama bora, ukanifunza kuwa na bidii na ulinifunza haya yote kwa njia ya kuwa hapa.

Also Read
Mamito apeleka ucheshi nchini Tanzania

Mimi sio mkamilifu, lakini kwako ninajaribu kuwa bora zaidi. Tabasamu lako hunipa amani ya milele, uwepo wako hunipa raha isiyo kifani.

Naomba Allah akubariki na kwa njia nyingi kwa miaka mingi ijayo na ujue mimi mamako niko nawe daima liwe liwalo.”

Hamisa Mobetto, mwanamitindo wa Tanzania ambaye pia ana mtoto wa kiume na Diamond ali comment kwa post ya Donna na aliandika, “Happiest birthday to mtoto wetu, Tunakupenda sanaaaah”

Also Read
Tanzania waikomoa Somalia 8-1 na kutinga nusu fainali ya Cecafa

Tanasha na Mobetto wana uhusiano mwema na hivi maajuzi walionekana kuwa na mipango ya kuwakutanisha watoto wao ambao ni ndugu.

Diamond hajaandika lolote Instagram kuhusu siku ya kuzaliwa kwa mwanawe Naseeb. Post yake ya mwisho ni ya kazi ya kampeini ya kumpigia debe Rais John Pombe Magufuli anayewania kipindi cha pili cha uongozi kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu kupitia chama cha CCM.

  

Latest posts

KFCB Yazuia Usambazaji Wa Filamu

Marion Bosire

Eduswagga Azungumzia Safari Yake Ya Muziki

Marion Bosire

Tory Lanez Afuta Instagram Kulikoni?

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi