NCCK yahimiza mwafaka Kati ya idara ya Mahakama na Serikali kuu

Baraza la makanisa nchini NCCK, limetoa wito kwa rais Uhuru Kenyatta na jaji mkuu Martha Koome, kuwasiliana na kutafuta muafaka kuhusu tofauti zilizopo baina ya idara ya mahakama na ikulu.

Katibu mkuu wa baraza hilo Chris Kinyanjui, alionya kwamba tofauti zinazodhihirishwa na pande hizo mbili, zitachangia migawanyiko nchini.

Also Read
KEMRI na JKUAT zashirikiana kutayarisha chanjo dhidi ya Covid-19

Baraza hilo pia limeongeza kwamba nipe nikupe baina ya asasi hizo mbili za serikali, haina manufaa yeyote, na ni mfano mbaya kwa udumishwaji wa sheria.

Also Read
IEBC yatangaza tarehe ya chaguzi ndogo za Garissa, Bonchari na Juja

Huku ikisalia miezi 13 pekee kabla ya kuandaliwa uchaguzi mkuu nchini, viongozi hao wa makanisa walitoa tahadhari dhidi ya jaribio lolote la kuahirisha tarehe ya uchaguzi mkuu.

Badala yake wamependekeza kwa tume ya uchaguzi nchini IEBC kuweka maandalizi ya uchaguzi wa mwaka 2022, kama suala la kipaumbele.

Also Read
Rais Kenyatta aombwa kufanya mabadiliko zaidi katika tume ya IEBC kabla ya uchaguzi mkuu wa 2022

Akizungumza katika sehemu tofauti, waziri wa kilimo Peter Munya, aliishtumu idara ya mahakama kwa kile alichosema ni mtindo wa kulazimisha mambo.

  

Latest posts

Justin Muturi kuwania urais kwa tiketi ya chama cha DP

Tom Mathinji

Bunge lapendekeza kuchunguzwa kwa mfumo wa ununuzi wa KEMSA

Tom Mathinji

Serikali yatoa chakula cha msaada kwa wanaokabiliwa na njaa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi