Ngirici aondoa kesi mahakamani kupinga ushindi wa Gavana Waiguru

Aliyekuwa muwaniaji kiti cha Ugavana kaunti ya Kirinyaga katika uchaguzi mkuu wa tarehe tisa mwezi Agosti Wangui Ngirici, ameondoa kesi aliyowasilisha mahakamani kupinga ushindi wa Gavana Anne Waiguru.

Kupitia kwa taarifa Ngirici alisema, “Baada ya kutafakari na mashauriano na wafuasi wangu na chama cha UDA pamoja na uongozi wa Muungano wa Kenya Kwanza, nimeamua kuchukua hatua ya kijasiri, ambayo haitanifaa au kumhujumu Gavana, lakini ambayo itawafaa kikamilifu watu wa kaunti ya Kirinyaga.”

Also Read
Maafisa wa afya waliofutwa katika kaunti ya Kirinyaga hawatarejeshwa kazini

Ngirici aliongeza kuwa, “Nimepitia dhoruba kali zikinishinikiza kuendelea na kesi hiyo, aidha nilichagua kuondoa kesi ya kupinga ushindi wa Gavana Waiguru, si ati sikuwa na ushahidi, lakini kuwapa fursa watu wa Kirinyaga kupata huduma bila kuvurugwa.”.

Also Read
Visa 156 vipya vya Covid-19 vyanakiliwa hapa nchini

Mwakilishi huyo wa zamani wa Kirinyaga alisema anampa Gavana Waiguru nafasi na fursa bila visingizio kutoa huduma kwa watu wa Kirinyaga pamoja na kutekeleza wadhifa wake wa mwenyekiti wa baraza la Magavana.

“Kuwahudumia watu wa Kirinyaga ni muhimu sana Kwangu kuliko ushindi wa kisiasa. kwa mawazo yangu, watu wa Kirinyaga daima watapewa kipaumbele. Kuna wakati mwingine wa kushinda,” alisema Ngirici.

Also Read
NCIC kubainisha maeneo hatari ya kukumbwa na ghasia za uchaguzi

Ngirici alisema sasa atamuunga kikamilifu Gavana kupitia mashauriano kila wakati kuhusu njia bora za kuwahudumia wakazi wa Kirinyaga.

Alimpongeza Gavana Waiguru, huku akimtakia afya njema anapotekeleza majukumu yake ya Ugavana.

  

Latest posts

Wabunge wa Kenya wawakwatua Wabunge wa Tanzania mabao 3-1

Dismas Otuke

EACC kutwaa Mali ya shilingi Milioni 216 ya afisa mmoja wa kampuni ya KETRACO

Tom Mathinji

Gavana Waiguru awaalika Wawekezaji katika Kaunti ya Kirinyaga

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi