Ngoma ya Burna Boy last last yagonga views milioni 4 nukta 7 ndani ya siku 10 pekee

Kibao kipya cha msanii wa Nigeria Damini Ebunoluwa Ogulu,maarufu kama Burna Boy kimefikisha views milioniĀ  4 nukta 7 diu 10 pekee baada ya kuwekwa kwenye mtandao wa You Tube .

Burna Boy aliye na umri wa miaka 30 ameweka video za maisha ya kifahari kwenye ukanda huo mpya yakiwa magari ,ndege na nyumba za kifahari na ameimba kibao hicho kwa lugha ya Igboo .

Also Read
Burna Boy na Stefflon Don bado wako pamoja

Katika video hiyo Burna anaonekana akilia huku akitiririkwa na machozi kitu ambacho ni adimu kwa wanaume wa Kiafrika kufanya hadharani.

Also Read
Princess Shyngle aomba ushauri mitandaoni

Burna pia ameimba juu ya kuvunjwa moyo na mpenzi wake huku ajiuliza mbona licha ya mahusiano kuvunjika ,aliyekuwa mpenzi wake anakataa kuchukua hata zawadi kutoka kwake.

Also Read
Burna boy ashukuru wote alioshirikiana nao

Video hiyo iliwekwa katika mtandao wa You Tube Mei 13 mwaka huu ,na kufikia mapema Jumatatu Mei 23 imerekodi views 4,740,687.

  

Latest posts

Mwigizaji Maina Olwenya Ameaga Dunia

Marion Bosire

Makundi ya wakiritimba yalaumiwa kwa kuficha Mahindi

Tom Mathinji

Visa 108 zaidi vya Covid-19 vyanakiliwa hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi