Ni sawa tu! Marioo

Mwanamuziki wa Tanzania Marioo ambaye juzi alizua kioja baada ya kuweka picha ya kitanzi Instagram na baadaye kutoa wimbo Asante na kitanzi ndicho picha ya cover ya wimbo huo amesema kwamba ni sawa tu ikiwa atakuwa na binti mrembo alafu Diamond amchukue.

Ikumbukwe kwamba wengi wa mashabiki walikisia kwamba Diamond ndiye sababu kuu ya Marioo kutoa wimbo huo ambapo anasikika kama ambaye amakata tamaa ya mapenzi kabisa.

Also Read
Kenya, Tanzania kuanzisha zoezi la pamoja la kuhesabu wanyamapori

Wengi wanasema Marioo amekuwa kwenye uhusiano wa mapenzi na Mimi Mars ambaye pia ni mwanamziki na ghafla Mimi Mars akaonekana kuwa karibu sana na Diamond Platinumz.

Sasa jana akihutubia wanahabari kuhusu kazi yake mpya kama balozi wa kampuni ya mavazi kwa jina “La Jouberg Classic Wear, (LJCW)” Marioo aliulizwa swali kuhusu uhusiano wa karibu wa Mimi Mars na Diamond akasema sio vibaya ikiwa Diamond atanyakua mpenzi wake.

Also Read
Diamond Amkumbuka Wema Sepetu

 

Kulingana naye Diamond ni nyota mkubwa ambaye amefanya mengi na ana nguvu ndio maana ana huo mvuto na jambo hilo litampa changamoto ajitume kazini sana ili naye afikie upeo kama wa Diamond.

Also Read
Diamond akiri Mzee Abdul Sio babake

 

Mario alipatiwa gari jipya na kampuni hiyo ya mavazi ya LJCW na wanapanga kuzindua duka jipya Dodoma ijumaa tarehe mbili mwezi Oktoba mwaka huu.

Akihojiwa Mimi Mars alisema uhusiano wake na Diamond ni wa kazi tu.

  

Latest posts

Wasanii Wanaowakilisha Kenya AFRIMA

Marion Bosire

Akothee Apata Mgeni wa Heshima Kwenye Hafla Yake

Marion Bosire

KFCB Yazuia Usambazaji Wa Filamu

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi