Ni watu wachache tu ambao wamejitokeza kusajiliwa kuwa wapiga kura

Tume ya uchaguzi nchini imeripoti kuwa ni watu wachache pekee waliojitokeza kusajiliwa kuwa wapiga kura katika juma la kwanza la shughuli hiyo.

Kufikia sasa ni wakenya 202,518 pekee waliojitokeza kusajiliwa kuwa wapiga kura wapya, badala ya wapiga kura milioni 1.5 kama iliyokuwa ikitarajiwa kila wiki.

Tume ya uchaguzi hapa nchini imesema hali hiyo imesababishwa na ukosefu wa usalama katika sehemu za kaunti ya Lamu, Baringo na Laikipia, na pia katia mpaka wa kenya na Somalia.

Also Read
Idadi kubwa ya wanariadha washiriki mkondo wa kwanza wa Track n field Nyayo

Swala la vijana kukosa vitambulisho vya kitaifa pia limetajwa kuchagia kwa idadi hiyo ndogo ya wanaosajiliwa kuwa wapiga kura.

Kaunti ya Samburu iliongoza kaunti nyingine kwa idadi ya wapiga kura wapya waliosajiliwa katika wiki ya kwanza ya zoezi hilo.

Tume ya uchaguzi iliwasajili wapiga kura wapya 2,128 badala ya lengo lake la wapiga kura wapya 27,059 katika kaunti ya Samburu ambayo ilifuatiwa na Elgeyo Marakwet ambapo wapiga kura wapya 3,889 walisajiliwa badala ya 58,856 waliolengwa.

Also Read
IEBC yahitaji shilingi bilioni 40 kuandaa uchaguzi Mkuu ujao

Kaunti ya Wajir ikiwa ya tatu kwa kuwasajili wapiga kura 3,489 badala ya 52,923 waliolengwa. Kaunti nyingine zilizowasajili wapiga kura zaidi ya elf tatu ni Pokot magharibi , Mandera, Nandi, Baringo, Narok, Turkana na Tana River.

Kaunti kumi zilizosajili idadi ndogo kabisa ya wapiga kura wapya ni pamoja na Mombasa, Nairobi, Kirinyaga, Embu, Laikipia, Muranga, Kitui, Nyandarua Nyeri na Kiambu. Nairobi na Mombasa zilisajili asili mia mbili pekee ya wapiga kura wapya waliokuwa wamelengwa.

Also Read
COVID-19: Afisi za Kaunti ya Kirinyaga zafungwa kwa muda

Kwenye taarifa,mwenyekiti wa tume hiyo ya Wafula Chebukati aliwahimiza wakenya kutumia fursa hii kujuiandikisha badala ya kusubiri hadi dakika zao mwisho kusajiliwa.

Zoezi hilo la mwezi mmoja linalenga kuwasajili wapiga kura wapya milioni sita.

  

Latest posts

Kenya Simbas yanusurika na kufuzu kwa fainali ya kombe la Afrika

DOtuke

Injera na Onyala kukosa nusu fainali ya Algeria baada ya kujeruhiwa

DOtuke

Makuzi ya Lugha ya Kiswahili

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi