Nick Cannon Azungumzia Afya Yake

Mchekeshaji na mtangazaji wa runinga Nick Cannon amesimulia safari yake ya maisha tangu abainike kuwa na ugonjwa wa Lupus. Kwenye kipindi chake kiitwacho “The Nick Cannon Show”, alielezea kwamba ni miaka 10 sasa tangu abainike kuugua Lupus, ugonjwa ambao ulisababisha abadilishe mtindo wake wa maisha kabisa.

Cannon alikumbuka wakati alijuzwa anaugua Lupus na kuelezea jinsi amekuwa akinakili hali yake ya afya kupitia video ambazo anarekodi akiwa nyumbani. Alionyesha video ya dakika sita ya jinsi amekuwa akifuatilia hali yake ya afya.

Also Read
Nick Cannon Aonyeshwa Heshima Kubwa Harlem, New York

‚ÄúSiku chache zilizopita nilikuwa nje kwenye theluji nikiwa na watu wa familia yangu tukicheza na kujivinjari ghafla nikaanza kufura mwili, sikuweza kupumua vizuri na maumivu makali kwenye upande wa kulia wa mwili wangu”. Alisema Cannon na kuongeza kwamba aliamka akajipata hospitalini akiwa amezungukwa na madaktari ambao walimbwambia kwamba figo yake ilikuwa na shida.

Also Read
Mipango ya mazishi ya mamake Koffi Olomide

Lupus ni hali ya kinga ya mwili kuvamia mwili ikidhania ni adui. Athari za ugonjwa huo hudhihirika kwenye sehemu tofauti za mwili kama vile ngozi, figo, seli za damu, ubongo, moyo na hata mapafu.

Also Read
Megan Thee Stallion Ahitimu

Video ya Cannon inaonyesha wakati mmoja akiambiwa na madaktari kwamba damu ilikuwa imeganda kwenye sehemu mbili tofauti za mapafu yake na maumivu kwenye figo.

Mchekeshaji huyo ambaye alikuwa mume wa mwanamuziki Mariah Carey, anasema kwamba hachukulii maradhi yake kuwa kitu kibaya bali anafurahia kwani anaweza kuelimisha umma na wengine ambao wanaugua maradhi sawia.

  

Latest posts

Rais Samia Alivyosherehekewa Kwenye Siku Yake ya Kuzaliwa

Marion Bosire

Azimio la Bien Barasa Mwaka Huu

Marion Bosire

Anne Kansiime Afiwa na Baba Mzazi

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi