Nigeria kuandaa fainali ya kombe la shirikisho baina ya vlabu mwaka huu

Shirikisho la kandanda Afrika CAF limetangaza kuwa uga wa Godswill Akpabio International mjini Uyo, Nigeria utaandaa fainali ya kombe la shirikisho msimu wa mwaka 2021/22 Ijumaa ya Mei 20 mwaka huu.

Itakuwa fainali kubwa ya Afrika kuandaliwa katika uwanja huo wa Godswill Akpabio ,ambao ni uwanja wa nyumbani wa klabu ya Akwa United inayoshiriki ligi kuu nchini Nigeria.

Also Read
Pitso Mosimane kukutana na waajiri wake wa zamani Mamelodi katika ligi ya mabingwa Afrika

Cotonou, Benin iliandaa fainali ya mwaka jana ambapo Raja Casablanca ya Moroko ilitawazwa mabingwa baada ya kuwacharaza JS Kabylie ya Algeria magoli 2-1.

Also Read
Dimba la AFCON kwa chipukizi chini ya miaka 20 kuanza Jumapili Mauritania

Marudio ya mechi za nusu fainali kupigwa Jumapili hii Mei 15 RS Berkane ikiwaalika TP Mazembe kutoka Jamhuri ya demokrasia ya Congo ,Mazembe wakiongoza bao 1 kwa bila kutokana na duru ya kwanza ,wakati Orlando Pirates wakiwa nyumbani dhidi ya Al Ahli Tripoli kutoka Libya,Pirates wakijivunia uongozi wa magoli 2 kwa nunge .

  

Latest posts

Serikali ya Uingereza yaidhinisha uuzaji wa klabu ya Chelsea kwa pauni bilioni 4 nukta 25

Dismas Otuke

Waakilishi wa Kenya ,Prisons na KCB wasajili ushindi wa pili mashindano Afrika kwa Voliboli ya vidosho

Dismas Otuke

Kenya na Zimbabwe zafungiwa nje ya mechi za kufuzu kombe la AFCON mwaka ujao nchini Ivory Coast

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi