Nigeria yadumisha rekodi ya asilimia 100 huku Misri pia ikifuzu raundi ya pili Afcon

Nigeria almaarufu Super Eagles ndio timu pekee iliyoshinda mechi zake zote katika hatua ya makundi ya Afcon ,baada ya kuwalemea Guinea Bissau mabao 2-0 katika mechi ya mwisho ya kundi D Jumatano usiku.

Magoli yote ya Super Eagles yalipachikwa kimiani kunako kipindi cha pili na Umar Sadiq na William Troost Ekong na kudumisha rekodi kuwa timu pekee mashindononi iliyoshinda mechi zake zote tatu.

Also Read
Justin Muturi kuwania urais kwa tiketi ya chama cha DP

Misri pia walisajili ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Sudan na kufuzu kwa raundi ya 16 bora.

Bao pekee la Misri lilipachikwa kimia i na Mohammed Abdelmonem kunako kipindi cha kwanza.

Also Read
Malkia Strikers wajizatiti lakini waanguka seti 3-0 mikononi mwa wenyeji Japan

Nigeria waliongoza kundi D kwa pointi 9 , wakifuatwa na Misri kwa alama 6 .

Mataifa yaliyotinga raindi ya 16 bora kwenye kindumbwendumbwe hicho ni pamoja na Cameroon na Birkina Faso kutoka kundi A,Senegal na Guinea kutoka kundi B,Morocco na Gabon za kundi C na Nigeria na Misri za kutoka kundi D.

Also Read
Tunisia na Mali zafuzu AFCON mwaka 2022 nchini Cameroon

Nafasi zilizosalia 7 za raundi ya pili zitabainaika Alhamisi kwenye mechi za mwisho za makundi ya E na F.

Raundi ya pili imeratibiwa kung’oa nanga Jumamosi na kukamilika Jumanne ijayo.

  

Latest posts

Martha Karua atajwa mgombea mwenza wa Raila Odinga

Tom Mathinji

Barkane na Pirates kukabana koo Ijumaa fainali ya kombe la shirikisho

Dismas Otuke

Kimeli na Cheptai waibuka mabingwa wa mbio za kilomita 10 za Bengaluru

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi