“Nitamheshimu milele”, Sarah kuhusu Harmonize

Sarah Michelloti ambaye ni mke wa mwanamuziki wa Tanzania Harmonize amesema kwamba ataheshimu Harmonize milele hata kama wana matatizo.

Wanandoa hao wawili walianza kukwazana mwezi huu wa Disemba mwaka 2020 baada ya Harmonize kukiri kwamba ana mtoto nje ya ndoa.

Jambo hilo lilimkasirisha sana Sarah ambaye alitangaza kupitia mitandao ya kijamii kwamba mtoto huyo sio wa Harmonize na hata akachapisha majibu ya vipimo vya ‘DNA’.

Also Read
Tukutane mahakamani!

Kwa hasira Sarah alisema kwamba amemwacha Harmonize. Juzi mwanadada huyo aliandika tena kwenye Instagram akikashifu wanaosema uwongo kuhusu uhusiano wake na Harmonize.

Ameghadhabishwa na wanaotumia kutoelewana kati yake na mume wake kwa manufaa yao wenyewe.

Also Read
"Serikali tafadhali mchukulie hatua!" Msizwa

Kulingana naye, huenda wakarudiana na Harmonize au wakaachana kabisa lakini ataendelea kumheshimu milele.

Sarah wa asili ya Italia anasema Tanzania ni kama nyumbani na anaheshimu na kupenda watanzania wote kwani ndio familia yake kwa sasa.

Harmonize yuko mjini Accra nchini Ghana kwa sasa na hajasema lolote kuhusu maneno ya mke wake Sarah. Lakini siku ya kutangaza wazi mtoto wake, Harmonize alimwomba Sarah msamaha huku akisema kwamba hangeweza kuendelea kuficha mwanawe kwa nia ya kulinda ndoa.

  

Latest posts

Filamu ya Kenya yashinda tuzo nchini Nigeria

Tom Mathinji

Just A Band yarejea tena baada ya kimya cha muda

Tom Mathinji

Yul Edochie Azungumzia Ndoa Yake ya Wake Wawili

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi