Njoro anaomboleza

Mchekeshaji George Maina maarufu kama Njoro, anaomboleza kifo chababake mzazi. Alitangaza hayo kupitia akaunti yake ya Instagram ambapo aliweka picha ya mshumaa yenye neno “R.I.P”.

Aliongeza maneno ya kuonyesha alivyovunjika moyo kutokana na kuaga kwa babake huku akijiuliza maswali mengi tu yasiyokuwa na majibu.

Watu kadhaa maarufu walimwandikia Njoro maneno ya kumtia moyo mchekeshaji huyo wa awali wa kipindi cha Churchill.

Mwanamuziki aliyepia muigizaji Pascal Tokodi alimwandikia, “Pole brother.”, na mtangazaji wa redio Massawe Japani akamwandikia, “It is well Njoro, condolences.”.

Mchekeshaji Daniel Ndambuki almaarufu Churchill aliandika, “So so sad poleni sana. I have been there and i know what you are going through. My condolenses.”

Mwezi Julai mwaka jana, alitangaza kwamba babake alikuwa anaugua saratani ya utumbo jambo ambalo lilimkwaza sana kiasi cha kukumbwa na msongo wa mawazo.

Njoro amekuwa akipitia mengi maishani siku za hivi karibuni na wakati ameanza kurejea kwenye hali nzuri anapata pigo la kupoteza babake mzazi.

Wakati huo wahisani walijitokeza ili kuchanga kusaidia kugharamia matibabu ya babake lakini shirika moja likajitolea kulipa gharama hiyo yote.

Shirika hilo kwa jina “Project Afya” husaidia watu ambao wanaugua na hawana uwezo wa kugharamia matibabu.

Njoro aliwahi kupata tatizo la msongo wa mawazo hadi akaingilia utumizi wa pombe na mihadarati mpaka alipojitokeza akasaidiwa kwa kupelekwa kwenye kituo cha kurekebisha tabia na alipotoka akapata kazi kama mtangazaji wa redio na runinga.

  

Latest posts

Hata Nikifa Wanangu Hawatateseka – Asema Akothee

Marion Bosire

Miaka 70 ya Uwepo wa Ukumbi wa Maonyesho ya Sanaa

Marion Bosire

Ringtone Atangaza Kwamba Ameacha Kuimba Nyimbo za Injili

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi