Shirika la huduma kwa Jiji la Nairobi (NMS), limeahirisha ufunguzi wa kituo cha magari ya uchukuzi wa abiria cha Green Park Jijini Nairobi.Kituo hicho kilikuwa kianze kuhudumu siku ya Jumanne.
Kwenye taarifa,shirika la NMS limesema uamuzi wa kuahirisha ufunguzi unafuatia ombi la wahudumu wa magari ya uchukuzi. Shirika hilo limesema tarehe mpya ya ufunguzi rasmi itatangazwa hivi karbuni.
“NMS ingependa kufahamisha umma kuwa shughuli za uchukuzi katika kituo cha magari ya uchukuzi cha Green Park, zilizokuwa zianze tarehe 24 mwezi Mei mwaka 2022, zimeahirishwa kufuatia ombi kutoka kwa wahudumu wa magari ya uchukuzi,” ilisema NMS kupitia mtandao wake wa twitter.
Wahudumu wa magari ya uchukuzi wa abiria walikuwa wamedai kuwa mradi huo uliogharimu shilling million 250 unafunguliwa bila kuwaarifu wahusika wote.
Mwenyekiti wa chama cha wamiliki wa matatu Simon Kimutai alisema serikali ilifaa kushugulikia kwanza maswala muhimu kama vile,kama vile sehemu za maegesho.
Hii sio mara ya kwanza shirika la NMS limeahirisha ufunguzi wa kituo hicho kuhusiana na malalamiko kutoka kwa wahudumu wa magari ya uchukuzi wa abiria.