NOCK yazindua maafisa watano wa kiufundi kuingoza Kenya kwa michezo ya Olimpiki

Kamati ya Olimpiki nchini NOCK imezindua maafisa watano wa kiufundi watakaoambatana na kikosi cha Kenya kwa michezo ya Olimpiki makala ya 32 mjini Tokyo Japan .

Maafisa hao ni pamoja na afisa mkuu wa matibabu Dkt Carole Akoth,mwanasaikolojia wa michezo Kanyali Ilako,mshauri wa tiba maungo
Geoffrey Kimani,mtaalamu wa sayanyi ya michezo Rosemary Owino na mtaalam wa lishe Mercy Barwecho.

Akiwajulisha maafisa hao Rais wa NOCK Dkt Paul Tergat amesema wamelazimika kuwateua maafisa hao kwa mara ya kwanza kutokana na kubadilika kwa hali ya michezo ya sasa inayojumuisha mambo mengi wakati wa mazoezi na maandalizi.

Also Read
Malkia Strikers waanza kambi ya siku nne Mombasa ya nyanda za chini

“Tumeona kuwa michezo ya sasa kinyume na kitambo imebadilika na inashirikisha sayansi ili kuimarisha uwezo wa mwanaspoti wakati wa mazoezi,na ndio maana tumewateua maafisa hawa kuandamana na timu kwenda Tokyo Japana kwa michezo hii “akasema Tergat .

Maafisa hao watawahudumia wanamichezo wote wa Kenya watakaoshiriki michezo ya Olimpiki baina ya Julai na Agosti mwaka huu.

Dkt Carole Akinyi ni tabibu wa wizara ya afya na mchezaji magongo mstaafu wa timu ya taifa na aliteuliwa kuwa tabibu mkuu wa timu ya Kenya ya Olimpiki mwaka uliopita na atasimamiia kikosi cha Kenya kwa maswala yote ya matibabu na afya.

Also Read
Mwanariadha Mark Otieno apokea ufadhili wa shilingi milioni 1 kutoka Safaricom

Kanyali Ilako ana tajriba ya kufanya kazi na wanasoka na wanariadha wa kulipwa ,sawa na waogeleaji na wachezaji walemavu hapa nchini na ughaibuni na alikuwa mwogelaji wa zamani wa timu ya taifa.

Rosemary Owino ni mwanasayansi wa michezo na kocha aliyehitimu wa Tennis akiongoza timu ya Kenya akiwa nahodha waiposhiriki mashindano ya Davis Cup .

Geoffrey Kimani ni mtaalamu wa tiba ya maungo akiwa na tajriba baada ya kuhudumia timu ya wachezaji 7 kila upande ya raga ,wanariadha na pia amefanya kazi na wachezaji soka.

Also Read
Shujaa kupiga kambi ya Mazoezi mjini Stellenbosch kwa siku 10
Maafisa hao watano wakiwa na Rais wa Nock Paul Tergat,(katikati) Meneja wa timu ya Kenya ya Olimpiki Barnaba Korir (wa pili kushoto) na kiongozi wa ujumbe wa Kenya Waithaka Kioni(pembeni kulia)

Mercy Barwecho,alikuwa mtaalam wa lishe kwa timu za taifa za Kenya katika mashindano mengi ikiwemo michezo ya Olimpiki ya London mwaka 2012 na ile ya Rio De Janeiro mwaka 2016 sawia na michezo ya jumuiya ya madola.

Maafisa hao wanaanza kutekeleza majukumu yao mara moja kwenye timu za wanariadha wa mbio za masafa mafupi na taekwondo zilizo kambini huku timu ya wanaume na wanawake katika raga ya wachezaji 7 kila upande zikitarajiwa kuingia kambini katika uwanja wa Kasarani wiki ijayo.

  

Latest posts

Wakenya Rotich na Tanui wavunja rekodi za Paris na Amsterderm Marathon

Dismas Otuke

Tusker waleweshwa nyumbani na Zamalek 1-0

Dismas Otuke

Tysa yasherekea miaka 20 ya kubadilisha vijana Kitale kupitia soka

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi