Noordin Haji ataka majaji watatu wasikilize kesi dhidi ya Henry Rotich

Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP), Noordin Haji, sasa anataka  majaji watatu wateuliwe kusikiza na kuamua kesi iliyowasilishwa na waziri wa  zamani wa  Fedha, Henry Rotich, kupinga mashtaka  dhidi yake  kuhusiana  na  kashfa ya mabwawa ya Kimwarer na Arror. 

Haji  kwenye taarifa  kwa   mahakama  anasema kesi dhidi ya Rotich ina maswali makubwa   ya   kisheria na yenye umihimu kwa  umma kwa hivyo  kuna haja   isikilizwe na  majaji watatu.  

Anataka majaji  hao wabaini  ikiwa Mawaziri hawawezi kushtakiwa kwa mashtaka ya jinai kwa sababu ya vitendo vyovyote na upungufu ambao unaadhibiwa na sheria wakiwa kazini.  

Waziri wa  zamani wa  Fedha, Henry Rotich, na watu  wengine wanne wanashutumiwa kwa  kuhusika na matumizi mabaya ya pesa za umma zinazohusiana na ujenzi wa Miradi ya Mabwawa  ya Aror na  Kimwarer.

Makosa hayo ni pamoja na kula njama za ulaghai, matumizi mabaya ya  mamlaka, na kutofuata masharti ya sheria wakati wa kutekeleza mikataba ambayo inataka serikali ya Kenya kulipa takriban Shilingi  bilioni 63  kwa ujenzi wa mabwawa hayo mawili.

Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma  wiki iliyopita ilipuuzilia mbali ripoti kwamba mashtaka dhidi ya waziri huyo  wa zamani wa Hazina yameondolewa.

  

Latest posts

Rais Kenyatta amwomboleza Nancy Karoney, dadake waziri wa ardhi Farida Karoney

Tom Mathinji

Ronald Koeman atimuliwa Barcelona baada ya kushindwa na Vallecano

Dismas Otuke

Mutahi Kagwe: Wahudumu wa afya wafeli katika somo la Kingereza

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi