Nyani wachanjwa dhidi ya Covid-19 San Diego

Nyani kadhaa katika hifadhi ya wanyamapori ya San Diego wamepewa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Covid-19 kwenye mpango wa majaribio.

Chanjo hiyo imetolewa baada ya kuripotiwa kuzuka ugonjwa huo miongoni mwa wanyamapori kwenye hifadhi hiyo.

Also Read
Uganda yakana madai kwamba viongozi wakuu serikalini wamechanjwa kisiri dhidi ya COVID-19

Nyani watano walipewa chanjo mbili zilizotengenezwa na kampuni ya Zoetis.

Kampuni ya Zoetis ambayo hutengeneza dawa na chanjo, iliwachanja wanyama hao katika hifadhi hiyo huku ikitaja chanjo hiyo kuwa haipaswi kutumiwa kwa wanadamu.

Also Read
Idadi ya visa vya COVID-19 vyatimia 96,908 baada ya watu 106 zaidi kuambukizwa

Aidha awali Sokwe wanane walipewa chanjo hiyo na kuwa wa kwanza duniani kupewa matibabu hayo mnamo mwezi wa Januari.

Habari zaidi zinasema nyani hao wameanza kupata nafuu.

Also Read
Shirika la Kenya Airways kusitisha safari zake za Uingereza tarehe 9 mwezi huu

Afisa mkuu wa hifadhi ya wanyamapori ya San Diego Nadine Lamberski alisema wanyamapori hao hawajakabiliwa na hatari yoyote tangu wapewe chanjo hizo na hiyo huenda ikawa ishara ya mafanikio ya chanjo hiyo.

  

Latest posts

Zimbabwe: Watumishi wa umma ambao hawajachanjwa dhidi ya COVID-19 waadhibiwa

Tom Mathinji

Jeshi la Uganda latoa onyo kali dhidi ya jaribio lolote la mapinduzi

Tom Mathinji

Rais Samia Suluhu Hassan afanya mabadiliko katika baraza la Mawaziri

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi