Nyanza yaongoza kwa ukusanyaji saini kuunga mkono BBI

Eneo la Nyanza ndilo limeongoza katika shughuli ya ukusanyaji saini kwa ule mchakato wa jopo la BBI likiwa limekusanya saini 780,427.

Wakiongea Alhamisi gavana wa Kisumu,Anyang Nyong’o na mwenzake wa Siaya,Cornel Rasanga, waliwapuuzilia mbali wale wanaohimiza kura ya maandalizi kuandaliwa wakati mmoja na uchaguzi mkuu mwaka wa 2022.

Also Read
Mwaniaji ugavana wa Kisii Rael Otundo aitaka serikali kuimarisha usalama mpaka wa Kisii na Tranz Mara

Naibu rais William Ruto na washirika wake Jumanne walihimiza kura ya maamuzi kuandaliwa pamoja na uchaguzi mkuu mwaka wa 2022 bila gharama yoyote.

Also Read
Watatu waangamia na wengine kupofuka kwa kubugia pombe haramu

Hata hivyo, Anyang Nyong’o na Rasanga walisisitiza kwamba wapiga kura watatatizika na mrundiko wa upigaji kura ikiwa shughuli hizo mbili zitaandaliwa wakati mmoja.

Katika eneo la Nyanza kaunti ya Kisumu iliongoza kwa saini 177,832, kaunti ya Homa Bay ilikusanya saini 174,603 ikifuatiwa na Siaya kwa saini 156,323.

Also Read
Bunge la Kaunti ya Murang’a kuchunguza madai ya dhuluma kwenye Kampuni ya Kakuzi

Eneo la Nyanza lilifuatiwa na eneo la mashariki kwa saini 761,776 na eneo la Rift Valley likawa la tatu kwa saini 667,731.

  

Latest posts

Dereva na Makondakta wawili watiwa nguvuni kwa kukiuka sheria za trafiki

Tom Mathinji

Watu wanne zaidi wameambukizwa Covid-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Matabibu wataka Uchunguzi wa mipakani kuimarishwa kuzuia kuenea kwa Ebola

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi