Obiri ajiondoa mbio za nyika Nandi Jumamosi

Bingwa wa dunia wa mbio za Nyika Hellen obiri amejiondoa kushiriki  mkondo wa pili wa mbio za nyika  Jumamosi hii katika kaunti ya Nandi.

Kulingana na Obiri aliyeshinda mkondo wa kwanza wa Machakos mapema mwezi ni kuwa atarejea kushiriki  mashindano ya mwezi ujao huko Ol kalou akitumia mashindano hayo kujiweka shwari   kushiriki michezo ya Olimpiki mwaka ujao kando na mashindano ya Diamond League.

Obiri akizungumza na KBC kwa njia ya kipekee anasema ameridhishwa na matokeo aliyosajili mwaka huu kuanzia  mwezi Septemba ambapo alitimka muda wa kasi katika mkondo wa Monaco katika mita 5000 kabla ya kuweka pia muda wa kasi katika mita 3000 mkondo wa Doha Diamond League na kuibuka mshindi  katika mashindano ya Kip Keino Classic Continental tour.

Also Read
Obiri afunga msimu kwa matao ya juu Kip keino Classic

“This year despite the pandemic nafurahia matokeo yangu ya kuweka muda wa kasi mara mbili na kushinda Kip Keino Classic”akasema Obiri

“Jumamosi sitakuwa Nandi kushiriki mbio za cross country ambazo lakini najitayarisha  kurejea Januari kushiriki mkondo wa tatu wa cross Country huko Ol Kalou ”

“Mwaka ujao nitalenga kushiriki mashindano kadhaa ya diamond league ,tutakaa chini tuzungumze na meneja wangu ndio tuone nitashiriki mashindano magani ya dimaond league, lakini my ultimate goal ni Olympics nikipata gold medal nitahamia road races,Olympic Gold ndio tu nakosa katika career yangu “akaongeza  Obiri

Also Read
Ethiopia yatinga AFCON2021 kwa mara ya 10 licha ya kupigwa 1-3 na Ivory Coast
Obiri akiwa katika mzunguko wa mwisho wa mita 5000 katika mashindano ya Kik keiino Classic

Wakati uo huo Obiri ambaye pia ni bingwa wa dunia katika mita 5000 ameiomba serikali kutenga fedha za kuwasaidia wanariadha waliostaafu baada ya kuiletea nchi sifa haswa kuwalipa kiasi fulani cha pesa za kujikimu na pia kuwawekea bima ya matibabu kama njia moja ya kuwapongeza na kutambua juhudi zao.

“Ukiandalia hawa wanariadha waliiletea Kenya sifa kwa kushinda mashindano,na njia ambayo naona ya kuwasaidia ni kwa serikali kuwalipa kiwango fulani cha pesa na pia kuwapatia Medical cover  ili wasitaabike sana”akaongeza Obiri

Also Read
AK imepiga hatua kubwa inapoadhimisha miaka 70

Obiri  ambaye ni Sajenti wa Laikipia Airbase katika jeshi aliyasema  haya alipohudhuria sherehe za kuadimisha miaka 70 tangu kubuniwa wka chama cha riadha Kenya Jumanne wiki hii katika uwanja wa taifa wa Nyayo.

Mbio za nyika za Jumamosi ambazo zitakuwa za mwisho mwaka huu zitashudia Sheilla Chepkurui akitimka kwa mara ya kwanza baada ya likizo ndefu huku pia Daniel Simiu akilenga kutwaa ubingwa wa pili mtawalia katika mbio za wanaume baada ya kushinda mkondo wa kwanza mjini Machakos.

  

Latest posts

Police Fc washerehekea kurejea ligi kuu baada ya mwongo mmoja kwa dhifa

Dismas Otuke

Sportpesa kurejesha ufadhili michezo nchini Kenya

Dismas Otuke

Vidosho wa Kenya wapigwa dafrao na Msumbiji mashindano ya kikapu Afrika

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi