Obiri awika Nyayo na kutwaa taji ya mita 5000 ,siku ya kwanza ya mashindano ya jeshi

Bingwa wa dunia katika mbio za mita 5000 Hellen Obiri kutoka Laikipia Air base amenyakua taji ya kitaifa ya shindano hilo la mizunguko 12 , katika siku ya kwanza ya makala ya 44 ya mashindano ya kikosi cha jeshi Jumatatu uwanjani Nyayo.

Obiri ambaye pia ni mshindi wa medali ya  fedha ya olimpiki katika shindano hilo aliongoza kutoka mwanzo hadi mwisho na kukata utepe kwa dakika 15 sekunde 22 nukta 64 ,ikiwa mara ya kwanza kutwaa taji hiyo  tangu mwaka 2017.

Also Read
Wanariadha 6 wanufaika na msaada wa masomo kutoka kwa ANOCA

Joyce Chepkemoi alimaliza katika nafasi ya pili kwa dakika 15 sekunde 23 nukta 36  huku Sheila Chepkurui   akiridhika katika nafasi ya tatu kwa dakika 15 sekunde 28  nukta 01  akifuatwa na Nespin Chepleting katika nafasi ya nne naye  Joycilline Jepkosgei  aliyekuwa akitetea taji aliyotwaa mwaka 2019 akiambulia nafasi ya tano.

Also Read
Uwanja wa Bin Ali utakaondaa kipute cha kombe la dunia mwaka 2022 wazinduliwa

Obiri  amesema mbinu alizotumia kwenye mashindano ya Jumatatu itamsaidia anapoelea kushiriki mashindano ya Diamond League mkondo wa Doha Mei 28 ,akijaribu kutetea taji ya mbio za mita 3000 .
Collins Koros wa Kahawa Barracks alinyakua ushindi wa mita 10,000 alipotumia dakika 28 sekunde 39 nukta 03 akifuatwa na Alfred Barkach kwa dakika 28 sekunde 42 nukta 5 huku Abel Mutai akimaliza wa tatu kwa dakika 28 sekunde 48 .
Mshikilizi wa rekodi ya dunia ya nusu marathon Kibiwott Kandie hakushiriki shindano hilo.
Mashindano hayo yataendelea siku ya Jumanne huku yakikamilika Jumatano ambapo jeshi wanayatumia kuteua kikosi chao kwa majaribio ya kitaifa ya olimpiki kati ya Juni 17 na 19 .
  

Latest posts

Kennedy Obuya asimulia jinsi mchezo wa Ckricket ulivyobadilisha maisha yake

Dismas Otuke

Mashindano baina ya mabunge ya Afrika Mashariki yaanza kutifua vumbi Arusha

Dismas Otuke

Omanyala ajiunga na National Police Service

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi