Obiri na Kandie wanyakua ubingwa wa mbio za nyika za KDF

Bingwa mtetezi wa dunia katika mbio za nyika  Hellen Obiri na mshikilizi wa rekodi ya dunia katika mbio za nusu marathon  Kibiwott Kandie waliongoza kutoka mwanzo hadi mwisho na kutwaa ubingwa wa  makala ya 40 ya mbio za nyika za kikosi cha KDF Ijumaa katika uwanja wa Moi Air base.

Obiri  ambaye alipokonywa taji ya mbio hizo mwaka jana kwa  Sheilla Chekurui  kutokana na jeraha la muda mrefu ,alidhihirisha umahiri wake  akiwa katika kundi la uongozi kutoka mwanzo  na kunyakua  nafasi ya kwanza  ya shindnao hilo la kilomita 10 kwa dakika 33 sekunde 25 nukta 1, akifuatwa na  senior private  Joyce Chepkemoi kutoka Laikipia kwa dakika 33 sekunde 32 nukta 6 naye Chepkurui  kutoka Thika akaridhia nafasi  ya tatu kwa dakika  33  na sekunde 47.

Also Read
Wakenya kutoana jasho mbio za Istanbul Half marathon Jumapili

Bingwa huyo wa dunia wa mita 5000 ambaye ni Sajenti katika kambi ya  Laikipia air base  amesema kuwa atashiriki mashindano ya kitaifa ya mbio za nyika Februari 13  huku akitangaza kujiondoa kwa mashindano ya mbio za nyika barani Afrika mjini Lome Togo mwezi machi mwaka huu.

“Mbio za leo zimekuwa ngumu ambapo nilikuwa napambana na mshindi wa mwaka jana lakini nafurahia ushindi na sasa nalenga kuiwakilisha KDF katika mashindano ya kitaifa mwezi ujao ingawa sitashiriki mashindano ya nyika barani Afrika”akasema Obiri

Also Read
Jebitok,Kipyegon na Chebet wafuzu kwa nusu fainali ya mita 1500

Nesphine Chepleting wa Isiolo aliibuka wa nne naye Irene Kamais wa kambi ya  Thika akaambulia nafasi ya tano.

Mbio za wanaume za kilomita 10  zilishindwa na  Gunner  Kibowott Kandie kutoka kambi ya Embakasi ambaye alihifadhi taji yake ya mwaka jana kwa dakika  29 sekunde  24 nukta 5 ,akifuatwa na  Collins Koros kutoka  Kahawa kwa dakika  29 sekunde 32 nukta 5 , huku  Erick Kiptanui wa Embakasi akiibuka wa tatu kwa dakika  29  sekunde 40 nukta 5 .

Kandie Kibiwott akikata utepe mbio za kilomita 10

Kandie amesema analenga kujikatia tiketi kwa mashindano ya Afrika huku pia akijitayarisha kwa michezo ya Olimpiki.

“Nitakuwa nikitafuta tiketi ya mashindano ya nyika Afrika,na pia nataka kushiriki michezo ya Olimpiki  mwaka huu”akasema Kandie

Also Read
Riadha Kenya kufunga afisi zao Ijumaa kutoa heshima kwa Agnes Tirop

Joseph Karanja na Vincent Mutai wa  Isiolo na  Kahawa waliambatana katika nafasi za 4 na 5 kwenye usanjari huo.

Obiri  pia aliingoza timu yake ya  Laikipia airebase  kunyakua ushindi katika mbio za kupokezana kijiti ,licha ya kuchukua kijiti akiwa katika nafasi ya 4.

KDF ilitumia mashindano hayo kuteua kikosi kitachoshiriki mashindano ya kitaifa mwezi ujao katika uwanja wa Ngong Race Course  ambapo chama cha riadha Kenya kitachagua timu itakayoshiriki mashindano ya nyika barani Afrika mjini Lome Togo kati ya Machi 6 na 7 mwaka huu.

 

  

Latest posts

Kenya Simbas yanusurika na kufuzu kwa fainali ya kombe la Afrika

DOtuke

Injera na Onyala kukosa nusu fainali ya Algeria baada ya kujeruhiwa

DOtuke

KBC yafadhili timu ya magari itakayoshiriki mashindano ya Machakos Rallycross

DOtuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi