Obiri,Chepkoech,na Cheruiyot miongoni mwa mabingwa 12 watakapoambana Doha Diamond league Ijumaa

Mabingwa watetezi 12 wa dunia watarejea mjini Doha Qatar IJumaa usiku Mei 28 katika mkondo wa pili wa dioamond league ,yapata miezi 20 tangu watwae dhahabu za dunia.

Bingwa wa Olimpiki katika mita 1500 Faith Chepng’etich Kipyegon  atafungua ukurasa atakapotimka mbio za mita 800  kuanzia saa tatu na dakika 14 usiku akipambana na bingwa wa zamani wa Afrika Rababi Arafi wa Moroko,Habitam Alemu wa Uhabeshi,Winnie Nyanyondo wa Uganda na Mmarekani Hannah Green.

Also Read
Simiyu arejea kuifunza Kenya

Timothy Cheruiyot ambaye ni bingwa wa dunia katika mita 1500 atarejea mjini Doha mwaka mmoja unusu baadae , akijaribu bahati katika shindano hilo ,baada ya kupona jeraha , akipata ukinzani kutoka kwa wenzake Bethwel Birgen,Vincent Kibet na Timothy Sein wakikabiliana na Ronald Musagala kutoka Uganda na mshindi wa nishani ya shaba ya dunia Sofiane El Bakkali kutoka Moroko ,fainali hiyo iking’oa nanga saa tatu na dakika 28.

Bingwa na mshikilizi wa rekodi ya dunia ya mita 3000 kuruka viunzi na kidimbwi cha maji Beatrice Chepkoech atawania taji hiyo  dhidi ya wenzake  bingwa wa zamani wa dunia Hyvin Kiyeng ,bingwa wa Afrika kwa chipukizi Fancy Cherono,bingwa wa dunia kwa chipukizi Norah Jeruto   na bingwa wa olimpiki kwa chipukizi Rosefline Chepng’etich  wakipimana ubabe na bingwa wa dunia mwaka 2017 Emmah Corbun wa Marekani  na  Mekkides Abeba wa Uhabeshi.

Also Read
Shehena ya kwanza ya vifaa vya mashindano ya dunia ya riadha ya U-20 yatua nchini

Fainali hiyo inayotarajiwa kuwa ya kusisimua itaanza saa nne kasoro dakika 7 usiku.

Also Read
Kenya Cup kuingia mzunguko wa pili Jumamosi

Bingwa wa dunia katika mita 5000 Hellen Obiri atajitosa katika fainali ya mita 3000 ikiwa pia miezi 20 tangu ashinde dhahabu ya dunia na atashindana na wakenya wenza Margaret Chelimo,Winny Chebet,Eca Cherono,Beatrice Chebet,Lillian Kasait na Sheila Chelangat,fainali hiyo ikianza kutimua vumbi saa nne na dakika 48 usiku.

Shindano la mwisho ni fainali ya mita 3000 kuruka viunzi na maji wanaume kuanzia saa tano na dakika 10 usiku Moses Kipsang akiwa mkenya pekee uwanjani.

  

Latest posts

Bayern Munich wapokea kichapo cha kihistoria 5-0 dhidi ya Borusia Monchengladbach na kutemwa nje ya kombe la DFB

Dismas Otuke

Ronald Koeman atimuliwa Barcelona baada ya kushindwa na Vallecano

Dismas Otuke

Droo ya Safari Sevens yatangazwa Mabingwa watetezi Morans wakikutanishwa na Uhispania

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi