Olu Jacobs, muigizaji mkongwe nchini Nigeria

Mwezi wa sita mwaka huu wa 2020 habari za kifo cha Oludotun Baiyewu Jacobs maarufu kama Olu Jacobs ambaye ni muigizaji wa muda mrefu nchini Nigeria zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii ila baadaye zilibainishwa kuwa za uongo.

Msemaji wa kundi la waigizaji nchini Nigeria Monalisa Chinda – Coker ni mmoja wa wale ambao walijuza ulimwengu ukweli kuhusu Olu Jacobs wakati habari za uwongo zilienea. 

 

Also Read
Teni alivyomfuata Davido usiku ili kupata Colabo!

Olu Jacobs ameachia picha za hivi karibuni zaidi kuashiria kwamba yuko buheri wa afya.

 

 

Oludotun Baiyewu Jacobs alizaliwa tarehe 11 mwezi julai mwaka 1942, hivi sasa ana umri wa miaka 78 na ana tajriba ya uigizaji ya miaka zaidi ya arobaini.

Olu alisomea uigizaji katika shule ya “Royal Academy of Dramatic Arts” huko England ambako pia alianzia taaluma yake ya uigizaji.

Amewahi kushurikishwa kwenye filamu nyingi tu za uingereza na za nyingine ulimwenguni pamoja na michezo ya kuigizwa ya kuonyeshwa kwenye kumbi huko uingereza.

Uncle Olu, jinsi wengi wa wanaofanya kazi naye humuita, aliwahi kushinda tuzo la muigizaji bora wa kiume kwenye “African Movie Academy Awards” mwaka 2007 kati ya tuzo zingine.

Mke wake pia ni muigizaji anaitwa Joke Silva na wamekuwa pamoja tangu mwaka 1989 na wamejaliwa watoto. Wanandoa hao wana kampuni kwa jina Lufodo Group ambayo inahusika na maswala ya kutengeneza filamu na ina shule ya uigizaji pia.

  

Latest posts

Mwelekezi Sir Jacob Otieno Ameaga Dunia

Marion Bosire

Daddy Owen Azindua Albamu Mpya

Marion Bosire

Ogopa Wasanii, Kibao Kipya Cha Willy Paul

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi