Mshikilizi wa rekodi ya Afrika katika mita 100 Ferdinand Omanyala, aliandikisha rekodi mpya ya mmbio za International Castiglione Athletics Meeting uwnajani Zecchini mjini Groseto, Italia Jumapili usiku .
Omanyala, aliibuka mshindi huku akiweka muda mpya wa sekunde 10 nukta 11 ,akifuztwa na Arthur Cisse,wa Ivoru Coast aliyemaliza wa pili kwa sekunde 10 nukta 14 wakati Fostine Desalu wa Italia akiridhika na nafasi ya tatu kwa sekunde 10 nukta 33.
Omanyala pia baadae aliweka muda bora wa kibinafsi katika mita 200 wa sekunde 20 nukta 50 ,akivunja rekodo yake ya awali ya sekunde 20 nukta 90 ya Machi 4 mwaka 2020.