Omanyala Omurwa afuzu kwa nusu fainali ya mita 100 Olimpiki na kusawazisha rekodi ya kitaifa

Ferdinand Omanyala Omurwa amefuzu kwa nusu fainali ya mita 100 katika michezo ya Olimpiki huku akisawazisha  rekodi ya kitaifa ya sekunde 10 nukta 01  Jumamosi alasiri.

Omanyala anayeshiriki Olimpiki kwa mara ya kwanza ameibuka wa tatu katika mchujo wa tatu   akiziparakasa na kuandikisha historia kuwa Mkenya wa kwanza kushiriki nusu fainali ya mita 100 katika michezo ya Olimpiki.

Also Read
Kenya tayari kuukaribisha ulimwengu kwa mashindano ya vijana wasiozidi umri wa miaka 20

Andre De Grasse wa Canada aliongoza kwa sekunde 9 nukta 91 akifuatwa na Fred Kerly wa USA .

Also Read
Wenyeji Cameroon wafungua CHAN kwa ushindi

Omanyala atarejea uwanjani saa saba na robo adhuhuri ya Jumapili kutimka nusu fainali ambayo amejumuishwa  mchujo wa kwanza  pamoja na Usheoritse Itsekiri wa Nigeria,Reece Prescod wa Uingereza,Gift leotlela wa Afrika Kusini ,Yohan Blake wa Jamaica,Andre De Grasse wa Canada,Fred Kerly wa USA na Jimmy Vicaut wa Ufaransa.

Also Read
Kalekwa aitaka serikali kuruhusu kuanza kwa ligi kuu ya FKF

 

 

  

Latest posts

Omanyala aweka rekodi mpya ya Afrika ya mita 100 ya sekunde 9 nukta 77 Kip Keino Classic

Dismas Otuke

Wakenya walenga kulipiza cha Olimpiki katika mita 3000 kuruka viunzi na maji katika Kip Keino Classic

Dismas Otuke

Faith Kipyegon kufunga msimu nyumbani Kip Keino Classic

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi