Ombi la Sonko kutaka Hakimu Ogoti ajiondoe kesini lagonga mwamba huku akiagizwa kufanyiwa uchunguzi wa kiakili

Hakimu Mkuu wa mahakama ya kukabiliana na ufisadi Douglas Ogoti hatajiondoa kwenye kesi ya ufisadi ya shilingi milioni 10 inayomkabili aliyekuwa Gavana wa Kaunti ya Nairobi Mike Mbuvi Sonko.

Ogoti ametupilia mbali ombi la Sonko la kumtaka ajiondoe kwenye kesi hiyo akisema hakuna ushahidi wa kuonyesha alipendelea kwenye uamuzi wake wa awali wa kesi hiyo.

Also Read
Wizara ya Afya yathibitisha visa vipya 957 vya COVID-19 na maafa 11

Sonko alikuwa amelalamika mara kadhaa jinsi mahakama ilivyowashughulikia mashahidi miongoni mwa malalamishi mengine.

Ogoti pia amepitisha uamuzi kwamba kesi hiyo lazima iendelee. Hii ni baada ya Sonko kukosa kufika mahakamani awali kwa misingi ya kuwa mgonjwa.

Sonko ameshtakiwa kwa kuitisha hongo ya shilingi milioni 10 kutoka kwa kampuni ya Web Tribe Ltd kupitia kwa kampuni ya ROG Security Limited ili ipokee malipo yake kutoka kwa serikali ya Kaunti ya Nairobi.

Also Read
Gavana wa Garissa Ali Korane aachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni 3.2

Haya yanajiri huku mahakama ikiagiza Sonko afanyiwe uchunguzi wa kiakili ili kutathmini iwapo yuko imara kuendelea kujibu mashtaka.

Hii ni baada ya mahakama hiyo kuambiwa kwamba Sonko alipimwa na daktari wa Hospitali ya Aga Khan na kuonekana kwamba ana matatizo ya kiakili ambayo hayamruhusu kujibu mashtaka.

Also Read
Bunge la Seneti lapokea azimio la Kumtimua Sonko mamlakani

Kufuatia ripoti hiyo, mahakama imetoa agizo kwamba Sonko afanyiwe uchunguzi wa kiakili na mtaalamu wa maswala ya kiakili katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta.

 

  

Latest posts

Shule za umma zina uwezo wa kuandikisha matokeo bora iwapo zitajikakamua zaidi

Tom Mathinji

Musalia Mudavadi apuuzilia mbali dhana ya ma-‘Hustler’

Tom Mathinji

Wafungwa watoroka katika gereza la Nanyuki usiku wa manane

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi