Omolo asajiliwa na Erzrum BB yaUturuki

Kiungo wa Kenya Johanna Omolo amejiunga na klabu ya Buyuksehir Belediye Erzurumspor  inayoshiriki ligi kuu Uturuki  kutoka  Cercle Brugge  ya Ubelgiji ambako amecheza kwa mismu minne  iliyopita.

Omolo anatarajiwa kujumuishwa katika kikosi cha timu yake mpya Alhamisi itakapochuana na  katika kombe la Uturuki dhidi ya Alanyaspor.

Also Read
'Ghost' Mulee na wasaidizi wake waonyeshwa mlango Harambee Stars

Klabu ya Erzrum BB ilitangaza usajili wa kiungo huyo kupitia kwa mtandao wa twitter Jumatano usiku akiwa Mkenya pekee anayesakata soka ya kulipwa nchini Uturuki kwa sasa.

Also Read
Harambee Stars kuzindua uhasama na Rwanda Jumapili Jioni mjini Kigali

Hata hivyo kiung huyo anakabiliwa na kibarua kigumu cha kuisaidia Erzrum BB kusalia ligini msimu ujao wakiburura mkia kwa alama13 baada ya michuano 18.

Omolo atakuwa mchezaji wa pili kutoka Afrika Mashariki kupiga soka ya kulipwa nchini Uturuki baada ya Ally Mbwana Samatta ambaye ni nahodha wa Tanzania kusajiliwa na Fernabahce mwanzani mwa msimu.

Also Read
Harambee Stars yasajili ushindi wa pili baada ya kuipiga kumbo Taifa Stars 2-1

 

 

 

 

 

  

Latest posts

Shujaa yaangukia kundi moja na Uhispania,USA na Chile mkondo wa Edmonton 7’s

Dismas Otuke

Tegla Lorupe balozi wa amani kupitia michezo

Dismas Otuke

Kenya Lionesses kuvaana na Msumbiji kuwania tiketi ya robo fainali FIBA Afrobasket

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi