Ongezeko la mikutano ya kisiasa huenda ikazidisha maambukizi ya Covid-19

Wataalam wa kimatibabu sasa wanaonya kwamba kutakuwa na ongezeko la maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 kutokana na kuongezeka kwa mikutano ya kisiasa nchini.

Tayari kaunti ya Nairobi na kaunti jirani ya Kiambu zimerekodi ongezeko la visa vya maambukizi hayo baada ya wapigaji kura wa Kiambaa kushiriki kwenye uchaguzi-mdogo wa kumchagua mbunge mpya.

Also Read
Watu 1,130 zaidi waambukizwa Covid-19 hapa nchini

Haya yanajiri baada ya shirika la afya duniani kuanzisha shughuli ya kutathmini masharti dhidi ya ugonjwa huo hususan jinsi ya kuwashughulikia wagonjwa walioambukizwa ugonjwa huo kutokana na maambukizi mapya.

Akiwahutubia wana-habari, Dkt. Loice Ombajo, ambaye ni afisa mkuu wa kitengo cha kushughulikia magonjwa yasiyo rahisi kuambukizana kwenye hospitali kuu ya Kenyatta, alisema kuna hali ya wasi-wasi kuhusiana na mikutano ya kisiasa ambapo watu hutangamana.

Also Read
Serikali yabuni kamati yakushughulikia Usalama na Utangamano wa umma

Kwa upande wake, afisa mkuu wa kitengo cha kuzuia magonjwa ambayo husambaa kwa urahisi Dkt. Joyce Onsongo, alikiri kwamba kuna ongezeko la visa vya maambukizi hayo kote ulimwenguni kutokana na maambukizi mapya yanayoibuka.

Also Read
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Jonson ajitenga kwa hofu ya maambukizi ya COVID-19

Siku ya Jumatatu Kenya ilinakili kiwango cha maambukizi ya virusi vya Covid-19 ch asilimia 8.2 baada ya kunakili  visa vipya 431 kutoka sampuli 5,218 zilizofanyiwa uchunguzi katika muda wa ma-saa 24.

  

Latest posts

Aden Duale: Uchaguzi Mkuu sharti uandaliwe tarehe 9 mwezi Agosti mwaka 2022

Tom Mathinji

Mudavadi asema taifa hili halipaswi kushuhudia ghasia kama zile za mwaka 2007

Tom Mathinji

Malkia Strikers wajizatiti lakini waanguka seti 3-0 mikononi mwa wenyeji Japan

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi