Ongezeko la visa vya Covid-19 nchini,lahujumu ufunguzi wa shule kikamilifu

Shule humu nchini huenda hazitafunguliwa kikamilifu kutokana na ongezeko la visa vya Covid-19 katika muda wa wiki chache zilizopita.

Akizungumza katika runinga ya KBC channel 1 Alhamisi, katibu mwandamizi katika wizara ya afya Dkt Mercy Mwangangi alisema kutokana na ongezeko la visa vya Covid-19 ni wanafunzi wa darasa la nne, darasa la nane na wale wa kidato cha nne ndio tu wataruhusiwa kuendelea na masomo.

“kutokana na hali ilivyo, tutaruhusu wanafunzi wa darasa la nne, darasa la nane na kidato cha nne na wale wanaofanya mitihani ya kitaifa huku tunapokadiria hali ilivyo,” alisema Mwangangi.

Also Read
Watu 98 zaidi wameambukizwa Covid-19 hapa nchini

Katibu huyo mwandamizi alidokeza changamoto iliyoko ya kuweka umbali unaohitajika miongoni mwa wanafunzi shuleni akisema taifa hili linapasa kujiandaa kuishi na virusi hivi.

Alitoa wito kwa wazazi kuwa watulivu huku wakihakikisha watoto wao wana vifaa vinavyohitajika. Aliwahimiza kuzingatia masharti ya wizara ya afya kukabiliana na covid-19.

Also Read
Uhaba wa barakoa wahatarisha maisha ya wanafunzi Naivasha

Wakati uo huo Dkt Mwangangi alitoa wito kwa wakenya kuzingatia kikamilifu masharti ya kudhibiti Covid-19 akionya kuwa kuna uwezekano wa kutokea kwa wimbi la pili la maambukizi hayo.

“Onyo la wimbi la pili lililotolewa na waziri wa afya linapaswa kuchukuliwa kwa makini sana. Wataalam wanatueleza hatufanyi vyema, maambukizi yanaongezeka,” alisema Mwangangi.

Alihusisha ongezeko la visa vya Covid-19 na kukosa kwa wakenya kutekeleza masharti ya wizara ya afya akisisitiza kuwa ugonjwa huo ungali nasi na ni vyema kujikinga.

Also Read
Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa yaonya kuhusu kiangazi Januari

“Watu 49 wamelazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi kutokana na Covid-19. Tunawasihi wakenya kama wizara kuvalia barakoa,kuosha mikono na kuzingatia mashsrti yote ya wizara ya afya,” aliongeza Dkt Mwangangi.

Kwa sasa watu 46,144 wameambukizwa Covid-19 hapa nchini huku maafa 858 yakisababishwa na virusi hivyo tangu mwezi Machi mwaka 2020.

  

Latest posts

Wanjigi: Kenya haina uwezo kuwapa wasio na ajira shilingi 6,000 kila mwezi

Tom Mathinji

Mwanaume ajitia kitanzi baada ya kuteketeza nyumba yake eneo la Gichugu

Tom Mathinji

Viongozi wa kaunti ya Murang’a wampendekeza Peter Kenneth kwa wadhifa wa naibu rais

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi