Onyesho la mitindo ya mavazi laahirishwa Rwanda

Onyesho hilo kwa jina “Mercedes Benz Fashion Week” lilikuwa limepangiwa kufanyika tarehe kumi mwezi Julai mwaka huu wa 2021 katika jiji kuu la Rwanda Kigali.

Lakini waandalizi wa onyesho hilo ambao ni kampuni za FCC Productions na Global Ovations walitoa tangazo tarehe mosi mwezi Julai mwaka 2021 kuashiria kuahirishwa kwa onyesho lenyewe hadi tarehe ambayo itatangazwa baadaye.

Also Read
John Mahama ajiondoa kuwa mjumbe maalum nchini Somalia

Kulingana nao, ongezeko la visa vya maambukizi ya virusi vya Corona ndiyo sababu kuu ya kuahirisha onyesho hilo na taarifa yao ilifuatia tangazo la serikali ya Rwanda la masharti mapya ya kudhibiti kusambaa kwa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Covid 19.

Waandalizi walikuwa wametilia maanani uwepo wa janga la Corona na walikuwa wamepanga kwamba hawangekuwa na umati wa kushuhudia onyesho hilo moja kwa moja ila lingepeperushwa moja kwa moja kupitia runinga. Mikutano ya hadhara imepigwa marufuku nchini Rwanda kwa sababu ya tandavu ya Corona.

Also Read
Ufaransa yaazimia kuboresha uhusiano wake na Rwanda

Onyesho la mitindo ya mavazi la Mercedes Benz lilianza mwaka 2019 jijini Kigali nchini Rwanda, kisha likaelekezwa nchini Ghana mwaka 2020 na awamu ya tatu itakuwa nchini Rwanda tarehe ambayo itatangazwa baadaye.

Also Read
RMD

Onyesho la mwaka huu lingehusisha wabunifu wa mitindo ya mavazi 15, watatu wa taifa la Rwanda, watatu kutoka Marekani, mmoja kutoka Ubelgiji, mmoja kutoka Ecuador, wawili kutoka Ghana, mmoja kutoka Afrika Kusini na mmoja kutoka Uingereza kati ya wengine.

Waandalizi wanasisitiza kwamba onyesho limeahirishwa na wala sio kutupiliwa mbali huku wakufuatilia jinsi janga la Corona linaendelea nchini Rwanda.

  

Latest posts

Rayvanny Kumtambulisha Msanii wa Kwanza NLM

Marion Bosire

Dulla Makabila Ajiondolea Lawama

Marion Bosire

Mwigizaji Atoa Ilani Kwa Rais Museveni

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi