Oooh Nyumbani ni nyumbani David Ouma ateuliwa naibu kocha wa SOFAPAKA miaka 8 baade

David Ouma ameteuliwa kuwa naibu kocha wa mabingwa wa ligi kuu mwaka 2009  Sofapaka inayoshiriki ligi kuu ya Kenya, akirejea kwenye timu hiyo kwa mara ya kwanza baada ya miaka 8.

Ouma ambaye mapema wiki hii amejiuzulu wadhfa wa kocha mkuu wa timu ya taifa ya wanawake Harambee Starlets  pia atatekeleza majukumu ya mkurugenzi wa michezo  kwenye klabu hiyo kando na kuwa naibu kocha.

Also Read
Bwenyenye wa Uingereza Nick Candy arusha ofa ya shilingi bilioni 374 kuinunua klabu Chelsea
Kocha Ouma akikaribishwa na Rais wa Sofapaka Elly Kalekwa

Ouma ambaye amekuwa kocha wa Starlets kwa miaka mitano iliyopita atakuwa msaidizi wa kocha mkuu Ken Odhiambo kutwaa mikoba ya Mike Mururi.

Also Read
Sofiane Bakali awasili Nairobi tayari kushiriki Kip Keino Classic

“Ouma amerejea nyumbani,nilijua siku moja atarejea mahali roho yake ipo.Alikuwa nasi kwa miaka mitano katika nyadfa tofauti  na alionyesha ari na mapenzi kwa kazi yake,na tulipopata fursa ya kufanya naye kazi tena hatukufikiria mara mbili “akasema Rais wa SOFAPAKA Elly Kalekwa

Also Read
Batoto Ba Mungu kuzindua uhasama na Tusker FC ligi kuu Ijumaa

  

Latest posts

Boro wamtimua meneja Chris Wilder kwa matokeo duni

Dismas Otuke

Malkia Strikers warejea nyumbani kinyemela baada ya kubanduliwa mashindano ya dunia

Dismas Otuke

CAF yafungua maombi ya maandalizi ya fainali za AFCON mwaka 2025

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi