Oparesheni ya kuwasaka wafungwa 6 waliotoroka gereza la Nanyuki laanzishwa

Kamishna mkuu wa magereza ya humu nchini Wycliffe Ogallo amesema uchunguzi umeanzishwa kuhusu kisa cha kutoroka kwa wafungwa 14 kutoka gereza la Nanyuki.

Akiongea baada ya kuzuru gereza hilo, Ogallo alisema kamishna wa eneo la Rift Valley ataongoza operesheni ya kuwasaka wafungwa 6 waliotoroka gereza hilo Jumamosi asubuhi.

Alitahadharisha WaKenya dhidi ya kuficha habari zozote kuwahusu wafungwa hao 6 ambao walikuwa wamehukumiwa kwa mauaji na wizi wa kimabavu na ambao amewataja kuwa hatari kwa wananchi wa kawaida.

Also Read
LSK kupinga kanuni za usalama kuhusu maandalizi ya mikutano

Alisema kwamba ni makosa kwa mfungwa yeyote kutoroka kifungo cha jela na kwamba iwapo watapatikana watashtakiwa tena kwa kosa la kutoroka jela.

Ogallo alizuru gereza hilo baada ya wafungwa 14 waliokuwa wamehukumiwa kwa makosa sugu kutoroka jela, lakini wanane kati yao walikamatwa tena, huku 6 wakiwa hawajulikani waliko hadi sasa.

Also Read
Serikali ya Kaunti ya Samburu yadaiwa kutumia shilingi milioni 147 kwa miradi ghushi

rearrested and six are still at large.

Siku ya Jumamosi afisa mkuu wa upelelezi wa kaunti ya Laikipia Onesmus Towett, alisema walisikia milio ya risasi kutoka kwa gereza hilo na walipoenda katika gereza hilo kukadiria hali, waliwakamata wafungwa wanane waliokuwa miongoni mwa waliotoroka.

Towett alisema polisi wanawasaka wafungwa sita ambao hadi sasa hawajulikani walipo, huku akitoa wito kwa umma kutoa habari kwa polisi zinazoweza kusababisha kukamatwa kwao.

Also Read
Kituo cha kudhibiti magonjwa Afrika chamsifu Rais Kenyatta kwa kufunga kaunti 5

Wafungwa sita ambao bado hawajapatikana ni pamoja na Mareri Tetkor kutoka Sipili,Rumuruti, Nangoye Lenawaso wa Wamba, Samburu, Lereiyo Lekiare kutoka Wamba, Samburu, wote wawili wakikabiliwa na mashtaka ya mauaji,  Francis Kamau wa Majengo, Nanyuki, Patrick Fundi wa Wamba, Samburu na James Sike kutoka Thome,.

  

Latest posts

Idara ya Mahakama yashutumiwa kwa kuhujumu shughuli muhimu za serikali

Tom Mathinji

Uhuru Kenyatta: Usalama wa taifa hili ni shwari

Tom Mathinji

Hospitali ya Kijeshi yazinduliwa katika kambi ya kijeshi ya Kahawa

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi