Orengo awasuta wanaopinga ripoti ya BBI

Kiongozi wa wachache katika bunge la seneti James Orengo amepuzilia mbali madai ya usimamizi wa shirika la Linda Katiba Initiative kwamba mchakato mzima wa marekebisho ya katiba ni mpango wa serikali, na badala yake akawataka wakenya kujiepusha na propaganda kama hizo.

Orengo alisema kwamba kamati iliyoongoza mchakato huo kupokea maoni ya wakenya kutoka sehemu tofauti ni Ushahidi wa kutosha kwamba ni shughuli iliyohusisha wananchi.  

Seneta huyo wa Siaya alisema utaratibu wa marekebisho ya katiba si lazima uendeshwa na mashirika ya kijamii ndio ubainishwe kuwa wa wananchi.

Aliwataka wanaopinga ripoti hiyo ya BBi kukoma kueneza propaganda kwa wananchi kuhusu yaliyomo kwenye ripoti hiyo.

“Wanapaswa kusitisha kuwapotosha wakenya ila wanapaswa kuelekeza juhudi zao katika yaliyomo kwenye ripoti hiyo,” alisema Orengo.

Orengo alikuwa akizungumza katika shule ya msingi ya Gem kaunti ya siaya ambako aliungana na mbunge wa sehemu hiyo Elisha Odhiambo na mbunge wa kaunti ya Siaya Christine Ombaka walitoa hundi za shilingi milioni 9.2 kwa vikundi tofauti.          

  

Latest posts

Mwanafunzi ateketeza bweni kukwepa kufanya mitihani Tharaka Nithi

Tom Mathinji

Mahakama yamzuia Mohammed Badi kuhudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri

Tom Mathinji

IEBC yalenga kuwasajili wapiga kura wapya milioni sita kabla Uchaguzi Mkuu ujao

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi