Nabulindo amrai Mudavadi kujiunga Raila katika Azimio la umoja

Mbunge wa eneo bunge la Matungu ,Peter Oscar Nabulindo,  amemtaka kiongozi wa chama cha Amani National Congress(ANC)  Musalia Mudavadi ,kujiunga na Raila Odinga kwenye muungano wa  Azimio la Umoja .

Nabulindo aliyechaguliwa mbunge wa Matungu kupitia chama cha ANC ,amesema ni wakati mwafaka na jambo la busara kwa Mudavadi kutoa mwelekeo wa chama mapema  kwa kujiunga  na Azimio la Umoja .

Kulingana na Nabulindo muda uliosalia kabla ya uchaguzi mkuu  ni mchache mno,  na itakuwa bora kwa ANC kuamua hatma yake kwa wafuasi na pia kwa wale wanaopanga kuwania viti kwa tiketi ya chama hicho.

Also Read
Mudavadi: Wakenya hawapaswi kushurutishwa kuunga mkono mwaniaji yeyote wa kisiasa

Nabulindo anahoji kuwa kiongozi huyo wa ANC atakuwa na fursa nzuri kuwa kwenye serikali ijayo akibuni muungano na Raila kuliko  kubuni muungano na chama cha UDA.

“Namwomba kiongozi wa chama changu kutoa msimamo na mwelekeo ,mapema na kuunda muungano na Raila katika Azimio la Umoja ,  ili watu wajipange maana ukiangalia muda uliosalia kabla ya uchaguzi ni mfupi sana”akasema Nabulindo

Mbunge huyo pia ametangaza kumuunga mkono Raila Odinga anayewania Urais kupitia azimio la Umoja ,akiwa mbunge wa pili wa ANC kufanya hivyo ,baada mbunge wa Lugari Ayub Savula kutangaza kuunga mkono Azimio la Umoja kwenye mkutano wa kisiasa ulioandaliwa uwanjani Bukhungu kaunti ya Kakamega tarehe 31 mwezi uliopita.

Also Read
Janga la Covid-19 limezidisha visa vya ukataji miti kwa njia haramu nchini

“Sijahama ANC ,bali ni kutangaza tu msimamo wangu kwani ukiangalia huku Matungu watu wengi wanaegemea muungano wa Azimio sawa tu na vile Ayub Savula pia alifanya na pia seneta Cleo Malala ambaye alitangaza kumuunga mkono naibu Rais William Ruto ” akaongeza Nabulindo

ANC imeiitisha kikao kikuu kwa wanachama wote nchini (NDC) katika ukumbi wa KICC tarehe 23 mwezi huu ambapo inatarajiwa kuwa Mudavadi atatangaza msimamo wa chama kwenye uchaguzi wa Urasi Agosti mwaka huu.

Kumekuwa na tetesi na minong’ono kuhusu hatma ya Mudavadi katika harakazi zake za kugombea Urais, wengine wakidokeza kuwa huenda akabuni mungano na chama cha United democratic Alliance(UDA) kinachoongozwa na Naibu Rais William Ruto.

Also Read
Muungano wa Mudavadi na Waiguru hautashinda uchaguzi wa Urais mwaka ujao

Mudavadi amekuwa kwenye muungano wa One Kenya Alliance (OKA) tangu mwaka uliopita huku wakisimama kidete kuwa wangali ndani ya OKA na wala hawana nia ya kugura.

Mudavadi amekuwa akishawishiwa sana na Ruto kubuni muungano na UDA ,huku kiongozi wa chama cha Wiper Stephen Kalonzo akidokezwa kuwa njiani kuunda muungano na muungano wa Azimio la Umoja chini ya uongozi wa Raila .

  

Latest posts

Kamati ya Kusaidia Rais Mteule Kuchukua Hatamu za Uongozi Yaanza Kazi Rasmi

Marion Bosire

Didmus Barasa Ajisalimisha kwa Maafisa wa Polisi

Marion Bosire

Gavana Mandago Sasa ni Seneta

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi