Oscar Sudi ajisalimisha kwa Polisi,asafirishwa Nairobi kuhojiwa na NCIC

Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi Jumapili asubuhi alijisalimisha kwa polisi baada ya kutafutwa na maafisa wa usalama kwa saa 48.

Sudi alijisalimisha katika kituo cha polisi cha Langas mjini  Eldoret akiwa ameandamana na wakili wake na mbunge wa kaunty ya Uasin Gishu, Gladys Shollei, mbunge wa Kimilili Didmus Barasa na naibu katibu mkuu wa chama cha jubilee Caleb Kositany miongoni mwa viongozi wengine wa sehemu hiyo.

Mbunge huyo kisha alisafirishwa kwa ndege hadi jijini Nairobi ambapo anatarajiwa kuandikisha taarifa na tume ya utangamano na mshikamano wa kitaifa NCIC

Also Read
Rais wa Tanzania Suluhu Hassan awasili Kenya kwa ziara ya siku mbili

Mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Uasin Gishu Gladys Sholei aliwahakikishia wakazi wa eneo bunge la Kapseret kwamba mbunge huyo yumo mikononi mwa maafisa wa usalama na atashughulikiwa kuambatana na sheria na tume ya mshikamano na utangamano wa kitaifa.

Mheshimiwa Sudi alijisalimisha kwa polisi kinyume na vyombo vya habari, hakukuwa na amri ya kukamatwa kwake na si ukweli alikuwa amejificha,”alisema Shollei.

Also Read
Muuaji sugu awahofisha wakazi wa Moi's bridge

Kamanda wa polisi kaunti ya Uasin Gishu Johnstone Ipara alithibitisha kujisalimisha kwa mbunge huyo wa Kapseret waliokuwa wakimtafuta tangu siku ya Ijumaa.

“Ni ukweli tumekuwa tukimsaka Oscar Sudi kutokana na matamshi aliyoyatoa siku ya Ijumaa. Hali ya taharuki iliyokuwepo katika eneo hili sasa imetulia baada ya mbunge huyo kujisalimisha,” alisema Ipara

Kundi la maafisa wa polisi likiongozwa na kamanda wa polisi katika kaunty ya Uasin Gishu ijumaa usiku lilifika katika makao ya Sudi kwa nia ya kumkamata kwa madai ya kutoa matamshi ya chuki.

Also Read
Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi ameachiliwa huru kwa dhamana

Juhudi zao ziligonga mwamba baada ya waliokuwa kwenye makao hayo kukataa kufungua lango na kundi la vijana kufunga barabara ziinazoelekea katika makao ya mbunge huyo.

Maafisa wa polisi waliingia kwenye makao ya mbunge huyo kupitia kwa ua ambapo mmoja wao alijeruhiwa kwa panga kwenye kidole gumba na mmoja wa raia.

Wakati wa kumtafuta Sudi, maafisa wawili wa polisi walijeruhiwa na watu watano kukamatwa

 

  

Latest posts

Mwanafunzi ateketeza bweni kukwepa kufanya mitihani Tharaka Nithi

Tom Mathinji

Mahakama yamzuia Mohammed Badi kuhudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri

Tom Mathinji

IEBC yalenga kuwasajili wapiga kura wapya milioni sita kabla Uchaguzi Mkuu ujao

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi