Otile Brown asajili msanii kwenye kampuni yake ya muziki

Mwanamuziki wa nchi ya Kenya Otile Brown kwa jina halisi Jacob Obunga amesajili msanii mwingine kwenye kampuni yake ya muziki kwa jina “Just in love Music”.

Msanii ambaye amesajiliwa anaitwa “Lexsil” jina la kikazi na jina halisi ni Alex Mosongo. Kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii, Otile aliomba mashabiki wake wamkaribishe Lexsil na wamfuate kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii.

Also Read
Nonini na Chipukeezy Wakutana Marekani
Lexsil na Otile afisini

Haijabainika ikiwa Lexsil ana kazi zake binafsi kabla ya usajili huo isipokuwa video fupi ya wimbo “Bam Bam” iliyochapishwa na “Bamming Music” na channel ambayo ina jina “Lexsil” kwenye youtube haina wimbo wowote. Kuna video fupi pia ambayo inamwonyesha akiimba na Otile.

Hili limetukia miezi kadhaa baada yake kupoteza msanii wa kwanza kuwahi kusajiliwa kwenye hiyo kampuni yake. Msanii huyo ambaye aliondoka ni binti ambaye anafahamika kama “Jovial”

Also Read
Brown Mauzo na Vera Sidika Kufunga Ndoa

Jovial ambaye sasa ana usimamizi mwingine, alikiri kwamba alikosa kuelewana na Otile jambo ambalo lilisababisha kuondoka kwake.

Inatazamiwa sasa kuona jinsi Otile atasimamia msanii Lexsil ikikumbukwa kwamba ndiye wa pili tu anapoanza biashara yake ya kusimamia wanamuziki.

Otile aliingia kwenye ulingo wa muziki nchini Kenya mwaka 2015. Alizaliwa Kisumu na akalelewa Mombasa na alipoanza kujulikana wengi walidhani anatokea Tanzania kwa sababu ya jinsi alikuwa akiimba na Kiswahili chake.

Also Read
Ushirikiano wa Koffi Olomide na Diamond Platnumz

Alizindua album yake ya kwanza kwa jina “Best of Otile Brown” mwaka 2017 na ya pili akaizindua tarehe tatu mwezi wa sita mwaka huu wa 2020 na inaitwa “Just in love”.

Uhusiano wake wa kimapenzi na mwanamitindo Verah Sidika ulisababisha Otile ajulikane zaidi haswa walipoachana.

Vera Sidika na Otile Brown

 

 

  

Latest posts

Filamu ya Kenya yashinda tuzo nchini Nigeria

Tom Mathinji

Just A Band yarejea tena baada ya kimya cha muda

Tom Mathinji

Yul Edochie Azungumzia Ndoa Yake ya Wake Wawili

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi