Pday Hurrikane Azungumzia Uhusiano Wake na Nyota Ndogo

Siku moja tu baada ya mwanamuziki wa Pwani Nyota Ndogo kutangaza kwamba mume wake amerejea na hana budi ila kuachana na mpenzi wake mwanamuziki Pday Hurrikane, Pday ameelezea uhusiano wao.

Akizungumza kwenye mahojiano na Kadzo Mungela kwenye kipindi cha runinga ya KBC cha Kudzacha, Pday alisema uhusiano wake wa kimapenzi na Nyota Ndogo unaanza ukiisha.

Wawili hao walikuwa na uhusiano wa kibiashara awali kabla ya kuingilia uhusiano wa kimapenzi mwezi Aprili mwaka huu. Pday anasema kila mara alipomzuru Nyota aligundua kwamba alikuwa anaumia kimapenzi Kwani mume wake mwingereza alikuwa amemnyamazia. Hapo ndipo mapenzi yaliota kati yao.

Also Read
Elynah Shiveka atuzwa Shujaa wa kaunti ya Kakamega

Hurrikane alikiri kwamba aliwahi kummezea mate Nyota Ndogo kitambo hata kama amemzidi umri. Alimsifia akisema ni mrembo na huwa hazeeki.

Also Read
Mtangazaji mashuhuri Badi Muhsin amefariki

Baada ya kuwa pamoja waliamua kurudia kibao ambacho kinaitwa “Ni Wewe”.

Pday mzaliwa wa kaunti ya Kilifi, alisema mume wa Nyota Ndogo amekuwa akimpigia simu kumwonya aachane na mke wake na kwamba amepiga ripoti polisi hadi akachoka.

Kwa sasa hali ya uhusiano wao haijulikani lakini anasema yeye ana mke na ikiwa Nyota Ndogo angekubali angemwoa awe mke wa pili.

Also Read
Rayvanny aomba msamaha

Kulingana na Nyota, Pday ndiye amesababisha mume wake Bwana Henning Nielsen,aseme naye tena ila amekuwa akimtumia pesa za matumizi kila mwezi.

Nyota Ndogo amemwomba radhi Pday Kwani anatembea peke yake kutangaza kazi yao ya muziki.

Nielsen aliondoka Kenya akarejea kwao na mwezi Aprili tarehe mosi, Nyota akamtania utani uliomtongea. Alimdanganya kwamba ana ujauzito jambo ambalo lilisababisha amnyamazie.

  

Latest posts

Ogopa Wasanii, Kibao Kipya Cha Willy Paul

Marion Bosire

Kipindi Cha Wendy Williams Kuendelezwa na Watangazaji Tofauti

Marion Bosire

“Upendo” Kibao Kipya Kutoka Kwa Zuchu Na Spice Diana

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi