Pembe za ndovu za thamani ya shilingi milioni 1.4 zapatikana kaunti ya Kajiado

Shirika la uhifadhi wanyama pori hapa nchini  KWS, limepata vipande vinne vya pembe za ndovu vilivyokuwa vimefichwa kichakani katika eneo la Kajiado ya Kati.

Afisa mkuu wa shirika hilo katika kaunti ya Kajiado Vincent Ongwae alisema vipande hivyo vya uzani wa kilo 14 na thamani ya shilingi milioni 1.4, vinashukiwa kuingizwa humu nchini kutoka taifa jirani kwani hakuna ndovu wamenakiliwa kuuawa humu nchini katika siku za hivi karibuni.

Also Read
Watu 120 wahofiwa kufariki katika mafuriko Ulaya Magharibi

“Wakazi walipata pembe hizo na kupiga ripoti kwa chifu ambaye alituarifu. Tunashuku pembe hizo ziliingizwa humu nchini kutoka taifa jirani ya Tanzania,” alisema Ongwae.

Hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo lakini uchunguzi unaendelea. Ongwae alisema shirika hilo limetoa shilingi milioni 13 kuwafidia wahanga wa mashambulizi ya wanyama pori katika kaunti ya Kajiado ambapo waathiriwa 65 kati ya mwaka 2014 na 2017 wameanza kupokea hela hizo.

Also Read
Mkutano wa ODM kufanyika Homa Bay licha ya marufuku dhidi ya mikusanyiko

Afisa huyo mkuu wa shirika la KWS aliongeza kuwa shughuli ya kuwafidia walioshambuliwa na wanyamapori baada ya mwaka 2017 inaendelea huku akiwataka walioathiriwa kuwa watulivu.

Also Read
Maafisa wa KWS wanasa mashua iliyotekeleza uvuvi haramu Tana River

“Wale waliofidiwa aidha walishambuliwa moja kwa moja na wanyamapori au waliopoteza mifugo baada ya kushambuliwa na wanyamapori kutoka mwaka 2014 hadi 2017. Wengine walioshambuliwa baada ya mwaka 2017 watafidiwa baada ya mchakato wa kuthibitisha visa hivyo utakapo kamilika,” alisema Ongwae.

  

Latest posts

Nyongeza ya bei za mafuta yapingwa Mahakamani

Tom Mathinji

Kenya yanakili visa 113 vipya vya COVID-19

Tom Mathinji

Wazazi wasema watatetea mtaala mpya wa Elimu wa CBC

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi