Peter Munya: Covid-19 ndio Chanzo cha bei ya juu ya mbolea

Na Kennedy Epalat.

Waziri wa kilimo Peter Munya amesema bei ya juu ya mbolea humu nchini imesababishwa na athari za ugonjwa wa Covid 19.

Munya aliyefika mbele ya kamati ya bunge la kitaifa kuhusu kilimo ili kueleza kinachosababisha bei ya juu ya mbolea humu nchini ikilinganishwa na mataifa mengine ya Afrika mashariki, alisema kupungua kwa dhamani ya shilling ya Kenya dhidi ya dola ya marekani na vita nchini Ukrain huenda vikasababisha kuongezeka zaidi kwa bei ya Mbolea humu nchini.

Also Read
Matiang'i: Serikali imeimarisha usalama katika mitaa duni

Munya aliiambia kamati hiyo kwamba bei za mbolea katika eneo la Afrika mashariki zinakaribiana, akiongeza kusema kwamba gharama ya chini ya kilimo nchini Uganda inatokana na kuwepo kwa mvua ya kutosha na wala sio nyenzo za kilimo.

Also Read
Shirika la Ndege nchini larejelea safari za ndege katika kaunti tano zilizokuwa zimefungwa

Hata hivyo alisema ingawa gharama ya kilimo nchini Uganda iko chini , bei ya mbolea nchini humo iko juu kuliko ilivyo nchini Kenya.

Also Read
Kikao maalum cha bunge la taifa chafutiliwa mbali

Wakulima wamelalamikia gharama ya juu ya kilimo humu nchini , na wakaihimiza serikali ipunguze bei ya mbolea ili waweze kuimarisha uzalishaji wa kilimo.

  

Latest posts

Kaunti za Isiolo na Siaya zamulikwa kwa ufujaji wa fedha

Tom Mathinji

Kalonzo: baadhi ya walioteuliwa kuwa Mawaziri si waadilifu

Tom Mathinji

George Kinoti amkabidhi mamlaka kaimu mkurugenzi wa DCI Hamisi Massa

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi