Klabu ya Police Fc iliyopandishwa ngazi kucheza ligi kuu ya Kenya msimu huu,imeanza ujenzi wa uwanja wa nyumbani Edward Mbugua akisaidiwa na mwenyekiti Nyale Munga na afisa mkuu mtandaji Chris. Onguso .
Uwanja huo unaomudu mashabiki 5000 unatarajiwa kukamilika kabla ya mwishoni mwa mwaka huu ,na itakuwa afueni kubwa kwa klabu hiyo ukiwaondolea gharama ya kulipia viwanja vya kufanyia mazoezi na kuchezea mechi za nyumbani .

Uwanja huo pia unajumuisha uwanja wa voliboli ,uwanja wa riadha ,jukwaa kuu na vyumba vya kubadilisha nguo na umegharamiwa na chama cha akiba na mikopo cha Police yaani Police Sacco.

Kwa mjibu wa Onguso uwanja huo utarajiwa kumalizika ndani ya miezi minne ,na sio tu timu za polisi zitaruhusiwa kutumia uwanja huo bali pia utakodiwa kwa timu za taifa na vilabu vingine.
Polisi Fc imewekeza pakubwa katika usajili wa wachezaji ikitwaa huduma za wanandinga kama vile Elvis Rupia, Francis Kahata, Duke Abuya, Clifton Miheso, John Mark Makwata, Musa Mohammed, Duncan Otieno na David Owino.