Police FC wanoa makali tayari kwa msimu mpya wa ligi kuu huku wakilenga taji

Klabu ya Police FC inalenga kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu mpya utakaoanza tarehe 27 mwezi ujao .

Kulingana na kocha mkuu Sammy Omolo wamerekebisha makosa ya safu ya ulinzi na ushmbuliaji ambayo ilikuwa hafifu msimu jana.

“Tumeangalia mahali tulimalizia msimu jana ambapo tulienda mechi 10 bila kufungwa na ndio maana tumeleta wachezaji watusaidie katika safu ya difense na ushambulizi ,pia tulikuwa tunaangalia mlinda lango ,lakini kupata mshambulizi imekuwa vigumu kidogo”akasema Pamzo

Also Read
El Bakkali ashinda dhahabu ya mita 3000 kuruka viunzi na kuzima ubabe wa Kenya tangu mwaka 1968

Omolo alisema kuwa wameanza mazoezi ya kutangulia msimu,huku akisitiza kuwa ufunguzi wa uwanja wa nyumbani kwa mechi za mpya wa mwaka 2022-2023 katika chuo cha mafunzo ya ujasusi mtaani South C, Nairobi.

“Uwanja yetu saa hii inaendelea vizuri na kujipanga itakuwa rahisi,maanake tutakuwa na uwanja wa nyumbani ,kuliko msimu jana ambapo tumekuwa tukilazimika kucheza mechi za numbani”

Kwa mjibu wa nahodha wa kikosi hicho Musa Mohammed wanaangazia kusajili matokeo mazuri msimu huu ,na wanapanga kuanza vyema msimu.

Also Read
Albert Wesonga ateuliwa meneja mpya wa AFC Leopards

“Pre season tumeanza vizuri kwa mazoezi na tunaomba tuanze ligi na tuimalize vizuri,kikosi naona kiko vizuri”akasema Musa

Mwenyekiti wa bodi ya Polisi Steve Isaboke amefichua kuwa wana mipango ya kuanzisha timu ya wanawake ambay siku moja itashiriki ligi msimu ujao.

“Leo tulikuwa tunakutana na wachezaji kwa mara ya kwanza tangu uteuzi wetu na mwenyekiti Nyale Munga ,na tuna mipango kuanzisha timu ya wanawake ambayo pia siku moja itashirik ligi kuu

Also Read
Posta Rangers wanyakua tuzo za mwezi Machi za ligi kuu FKF

tumezuru uwanja huu na tumeona uko karibu kukamilika na kile tunatarajia ni kuwa utaanza kutumika wakati msimu mpya wa ligi utakapoanza.Uwanja huu utatumika kwa michezo yote ya polisi ikiwemo riadha ,na uogeleaji na pia kuukodisha kwa timu nyingine ili kuwa kitega uchumi”akasema Isaboke

Uwanja huo umejengwa na shirika la akiba na mikopo la Police FC,na utamudu mashabiki zaidi ya elfu 5,000.

  

Latest posts

Malkia Strikers wabanduliwa mashindano ya dunia baada ya kipigo cha seti 3-1 na Puerto Rico

Dismas Otuke

Boubacar Kamara kutocheza kwa muda kutokana na Jeraha

Tom Mathinji

Familia ya Mbijiwe yatoa wito kwa Rais Ruto kusaidia kumpata mwana wao

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi