Polisi FC wazindua uzi mpya kwa mechi za msimu huu

Klabu ya Kenya Police FC iliyopandishwa daraja kucheza ligi kuu ya Kenya msimu huu inalenga kutwaa taji ya ligi kuu na wala sio tu kusalia ligini.

Mwenyeketi wa timu hiyo Nyale Munga amesema wanao uwezo wa kusajili wachezaji wenye haiba kuu na pia kuwalipa vizuri na hawako ligini kubahatisha bali kuwania ubingwa .

“sasa tumefanya usajili mzuri na tumeleta uzoevu na tunalenga kushinda mechi zote zilizosalia,tunalenga kufanya usajili wa mwisho leo baada ya hapo tutakuwa sawa” akasema Nyale Munga

Also Read
Wana Mvinyo Tusker na Afc leopards kufungua msimu wa ligi kuu ya KFK Jumamosi

“Polisi Fc tumeingia ligini kushindana na hakuna kurudi ,polisi fc mwanzo tunaweka maslahi ya wachezaji mbele na kuwalipa vizuri”akaongeza Nyale

Kocha wa Polisi John Bobby Ogolla kwa upande amefichua kuwa wanalenga kusalia ligini katika ,na wamerekebisha makosa waliyokuwa nayo katika mechi mbili za kwanza kabla ya kushinda Nzoia sugar Fc.

Also Read
Mabingwa wa NSL FC Tatanta waduwaza mabingwa watetezi wa ligi kuu Tusker FC 2-1

“Tulianza tukiwa chini katika games zetu mbili za mwanzo kabla ya kuimarika na kuishinda Nzoia Sugar katika mchuano wa tatu”akasema kocha Ogolla

Police Fc iliyopandishwa ligi kuu msimu huu kwa mara ya kwanza baada ya subira ya miaka 10 itachuana na KCB iliyomaliza ya pili ligini msimu jana katika mechi yao ya tatu ya ligi.

Benchi ya kiufundi ya Police Fc ikiongozwa na Bobby Ogolla

Nahodha wa kikosi hicho Musa Mohammed anasema amehiari kurejea nchini kutoka Lusaka Dyanamos ya Zambia ili kuitumikia Polisi FC n.

Also Read
Huduma za maji kukatizwa katika mitaa iliyoko barabara ya Waiyaki

“Kila game tutaichukua vile itakuwa,mkianza ligi huwa kuna shinda kadhha ya kucatch up,kila mechi ni ngumu sio tu KCB bali sisi pia tutajituma” akasema Musa Mohammed

Maafande hao tayari wamefanya usajili wa wachezaji wenye tajriba akiwmo mshambulizi wa zamani Ulinzi Stars Jonh Makwata,Clifton Miheso na Duncan Otieno.

 

 

 

 

  

Latest posts

Malkia Strikers wabanduliwa mashindano ya dunia baada ya kipigo cha seti 3-1 na Puerto Rico

Dismas Otuke

Boubacar Kamara kutocheza kwa muda kutokana na Jeraha

Tom Mathinji

Familia ya Mbijiwe yatoa wito kwa Rais Ruto kusaidia kumpata mwana wao

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi