Polisi waagizwa kutekeleza masharti ya kudhibiti Covid-19 kikamilifu

Polisi wameagizwa kutekeleza mikakati ya kuzuia msambao wa ugonjwa wa COVID-19 baada ya kuongezeka kwa visa vya maambukizi ya aina ya Delta ya virusi vya corona.

Inspekta Jenerali wa polisi Hillary Mutyambai, amesema amewagiza maafisa wote wakuu wa polisi kutekeleza marufuku dhidi ya mikusanyiko yote ya umma.

Also Read
Watu 18 zaidi wafariki hapa nchini kutokana na Covid-19

Mutyambai ametoa maagizo hayo baada ya waziri wa afya Mutahi Kagwe, kuwatahadharisha wakenya dhidi ya kulegeza kamba katika vita dhidi ya ugonjwa wa Covid-19.

Kwenye hotuba yake, Kagwe alifichua kuwa vituo vya afya kote nchini vimelemewa na idadi kubwa ya waathiriwa wa Covid-19 na kwamba vituo hivyo havina vitanda vya kutosha vya kuwalaza wagonjwa mahututi na vipumuzi.

Also Read
COVID-19: Watu 427 zaidi waambukizwa huku mgonjwa mmoja akiaga dunia

Kagwe aidha ameagiza halmashauri ya kusambaza dawa hapa nchini KEMSA kutoa vifaa vya kutosha vya kujikinga dhidi ya virusi vya corona kwa serikali za kaunti hata zile zilizo na billi ambazo hazijalipwa.

Also Read
Kenya kubuni kamati ya kusuluhisha mzozo wa kidiplomasia na Somalia

Serikali za kaunti pia zimetakiwa kuimarisha ujenzi wa mabomba ya hewa ya oksijen kwa maandalizi ya viwanda vya utayarishaji hewa ya oksijen ambavyo vitawekwa.

Waziri pia ametangaza kuwasilishwa hapa nchini kwa chanjo zaidi katika muda wa wiki mbili zijazo.

  

Latest posts

Idadi ndogo ya wakazi wa Nairobi wajitokeza kuchanjwa dhidi ya COVID-19

Tom Mathinji

Watumishi wa Umma wahimizwa kushirikisha taasisi mbali mbali kufanikisha majukumu yao

Tom Mathinji

Kenya yapokea dozi 200,000 za Sinopharm kutoka China

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi