Polisi waimarisha usalama kati kati mwa Jiji la Nairobi

Huduma ya taifa ya polisi imeimarisha usalama kati eneo la kati kati mwa Jiji la Nairobi ili kukomesha uhalifu.

Kamanda wa Polisi katika eneo la kati kati mwa Jiji la Nairobi Adamson Bunei anasema kwamba polisi watahaklikisha eneo hilo linabakia salama huku visa vya uhalifu unaotekelezwa na watu wakiwa kwenye Piki Piki vikitokomezwa.

Also Read
Serikali yatakiwa kuruhusu misaada ya kibinadamu kwa wakazi wa Kapedo

Bunei ambaye alikuwa akiongea ofisini mwake alisema maafisa walio na mavazi ya ki-raia tayari wamepelekwa maeneo mbali mbali ya Jiji na akahakikishia umma kwamba Jiji hilo sasa ni salama.

Also Read
LSK kupinga kanuni za usalama kuhusu maandalizi ya mikutano

Mkuu huyo wa polisi katika eneo la CBD alisema visa vya uhalifu unaotekelezwa na watu wakiwa kwenye Piki Piki sasda vimedhibitiwa baada ya doria kuimarishwa.

Hatua hiyo ya polisi inafuatia ongezeko la wizi unaotekelezwa na wahalifu ambao hujifanya kuwa wahudumu wa boda boda.

Also Read
Wito watolewa wa hatua kali kuchukuliwa dhidi ya wanasiasa wanaowatishia wanahabari

Mara nyingi wahalifu hao hulenga simu za rununu na mikoba ya wanaotembea kwa maguu na pia waendeshaji magari kabla ya kuondoka kwa kasi.

  

Latest posts

Idadi ndogo ya wakazi wa Nairobi wajitokeza kuchanjwa dhidi ya COVID-19

Tom Mathinji

Watumishi wa Umma wahimizwa kushirikisha taasisi mbali mbali kufanikisha majukumu yao

Tom Mathinji

Kenya yapokea dozi 200,000 za Sinopharm kutoka China

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi