Polisi waliomuua mwanamke katika bustani ya City wafungwa miaka 7 gerezani

Maafisa wawili wa polisi waliopatikana na makosa ya kuua bila kukusudia katika mauaji ya Jane Waiyaki katika bustani ya City mwaka 2018, wamehukumiwa kifungo cha miaka saba gerezani.

Maafisa hao walio na cheo cha Konstabo William Chirchir na Godfrey Kirui,hapo awali walikuwa wameomba wahukumiwe kufungo cha nje.

Hata hivyo, familia ya mwathiriwa ilipinga ombi hilo ikisema wanapaswa kufungwa ili iwe funzo kwa maafisa wengine wa polisi ambao hukiuka sheria.

Also Read
Kiwango cha deni nchini chafikia trilioni 7.1

Jaji wa mahakama kuu Stella Mutuku, alisema kuwa maafisa hao wa Polisi walitumia nguvu kupita kiasi walipomuua Janet Waiyaki katika bustani ya  City asubuhi ya tarehe 20 mwezi Mei mwaka 2018, na kumwacha mpwa wake Bernard Chege na majeraha mabaya.

Also Read
Washukiwa waliokamatwa kwenye karamu ya watoto ya Mountain View kuzuiliwa kwa siku saba

Jaji huyo alisema hakuna uhalifu wowote uliokuwa umetekelezwa na kwamba waathiriwa waliokuwa kwenye gari hawakuwa tisho kwa maafisa hao.

“Maafisa wote walikuwa na silaha na walipaswa kuwa makini sana. Ninaamini kulikuwa na mbinu mbadala za kuwatia nguvuni na pia walivunja sheria iliyowahitaji kulinda maisha”, alisema Jaji huyo.

Also Read
Huduma za maktaba kupitia mtandao kuzinduliwa hapa nchini

Mwanamke huyo aliyekuwa na umri  wa miaka  41 aliaga dunia huku mpwa wake wa miaka 26 akiachwa na majeraha mabaya baada ya gari walimokuwemo kumiminiwa risasi na maafisa hao wa Polisi katika bustani ya City siku hiyo ya mauti.

  

Latest posts

Mutahi Kagwe: Wahudumu wa afya wafeli katika somo la Kingereza

Tom Mathinji

Prof Magoha: Awamu ya kwanza ya ujenzi wa madarasa ya CBC kukamilika mwezi Aprili mwakani

Tom Mathinji

Benki ya dunia kuipa Kenya shilingi bilioni 16.7 kukabilia na ukame

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi