Polisi wamkamata mshukiwa wa mauaji ya mwanariadha Agnes Jebet

Mshukiwa wa mauaji ya mwanariadha Agnes Jebet Tirop  wenye umri wa miaka 25 ametiwa nguvuni na maafisa wa ujasusi.

Idara ya ujajusi DCI ilithibitisha kuwa Ibrahim Rotich ambaye alikuwa mpenziwe  Jebet, alikamatwa changamwe Jijini Mombasa katika kile maafisa hao wa polisi walisema alikuwa akijaribu kuingia katika nchi jirani.

Also Read
Polisi wawasaka wanafunzi 14 waliokuwa wakivuta bangi ndani ya matatu

“Mapema mchana mshukiwa huyo alihusika katika ajali ya barabarani alipogonga lorry katika eneo la Athi River katika barabara ya Mombasa alipokuwa akiwatoroka maafisa wa polisi,” ilisema DCI.

Also Read
Mwanabiashara wa Uturuki Harun Aydin arejeshwa kwao

Mshukiwa hiyo Kwa sasa anahojiwa na maafisa wa polisi katika kituo cha polisi cha Changamwe kabla ya kufikishwa mahakamani kushtakiwa kwa mauaji ya mwanariadha huyo

Also Read
Hit Squad yaingia kambini kujiandaa kwa mashindano ya Afrika mjini Maputo

Mwili wa Tirop ambaye aliwakilisha taifa hili katika mbio za mita 5,000 katika mashindano ya Olimpiki Jijini Tokyo ulipatikana Jumatano ndani ya nyumba yake Item, kaunti ya  Elgeyo Marakwet.

  

Latest posts

Dereva na Makondakta wawili watiwa nguvuni kwa kukiuka sheria za trafiki

Tom Mathinji

Watu wanne zaidi wameambukizwa Covid-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Matabibu wataka Uchunguzi wa mipakani kuimarishwa kuzuia kuenea kwa Ebola

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi