Polisi wampiga risasi na kumuua mtu mmoja kwa kutovalia barakoa Malaba

Wakazi wa mji wa Malaba waliandamana barabarani kwa siku ya pili baada ya mwanamme mmoja wa umri wa miaka 27 kudaiwa kuuawa kwa kupigwa risasi na polisi kwa kutovalia barakoa.

Ezekiel Odera, ambaye mwili wake ulipelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Kocholya alipigwa risasi kwenye kizuizi kimoja cha barabarani mwendo wa saa moja unusu Ijumaa usiku alipokuwa akirejea nyumbani kutoka kazini.

Also Read
Wakazi wa Narok wahimizwa kuchukua vitambulisho vyao kwenye Kituo cha Huduma

Wakazi waliwasha moto na kutoa barakoa zao na kusababisha msongamano mkubwa wa magari kwenye mji huo wa mpakani.

Wakazi hao waliokuwa na ghadhabu siku ya Jumamosi walikabiliana na maafisa wa polisi wa kitengo cha GSU mjini Malaba na viungani mwake.

Also Read
Wanafunzi 52 wa shule ya upili ya wavulana ya Kolanya kaunti ya Busia waambukizwa Covid-19

Viongozi wa eneo hilo akiwemo mbunge wa Teso kaskazini Edward Oku Kaunya alishtumu dhuluma za polisi na kutoa wito kwa Inspekta jenerali wa polisi Hillary Mutyambai kumkamata mhusika.

Akiwahutubia wanahabari jijini Nairobi, Kaunya ambaye pia ni naibu mwenyekiti wa kamati ya bunge kuhusu usalama na utawala alitoa wito kwa Inspekta jenerali na waziri wa usalama wa kitaifa Fred Matiangi kuwahamisha maafisa wote ambao wamehudumu kwa muda mrefu kwenye kaunti hiyo ndogo.

Also Read
Mwanaume atiwa nguvuni kwa kumbaka mwanafunzi wa kidato cha pili Malaba

Alisema kuwa katika muda wa miaka miwili iliyopita watu watatu wasio na hatia wameuawa kwa kupigwa risasi na polisi na hakuna yeyote aliyekamatwa huku akiwashtumu maafisa wa polisi kwa kuhusika katika uhalifu.

  

Latest posts

Wanjigi: Kenya haina uwezo kuwapa wasio na ajira shilingi 6,000 kila mwezi

Tom Mathinji

Mwanaume ajitia kitanzi baada ya kuteketeza nyumba yake eneo la Gichugu

Tom Mathinji

Viongozi wa kaunti ya Murang’a wampendekeza Peter Kenneth kwa wadhifa wa naibu rais

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi